read

22. Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Walipomtuhumu kumuuwa Uthman (r.a):

“Jihadhari! Kwa kweli shetani ameanza kuwahimiza watu wake, na amekusanya wenzake ili udhalimu urejee kwenye nafasi yake, na irejee batili kwenye kiwango chake. Wallahi hawajaniona na jambo ovu waka- likanusha, wala hawajafanya insafu kati yangu na wao.

Kwa kweli wao wanaidai haki ambayo wameitelekeza, na damu ambayo wameimwaga, ikiwa nilikuwa mshirika wao basi bila shaka wana hisa humo, na ikiwa wao ndio waliotenda bila ya mimi, kisasi kitakuwa juu yao tu. Kwa kweli hoja yao kubwa dhidi yangu iko dhidi yao wenyewe.

Wananyonyesha kwa mama alieacha kunyonyesha. Wanaihuisha bidaa iliyokwishauawa.
Oh! wee mdai usiyefanikiwa, njoo! Huu ndio wakati wako.1 Nani mdai? Na kwa lipi ameitikiwa? Mimi naridhika na hoja ya Mungu dhidi yao na ujuzi Wake kwao.”

Tishio la Vita!

“Endapo watakataa nitawakabili kwa makali ya upanga, ambao ni mponya- ji wa matendo batili na ni mnusuru wa haki. Yashangaza eti wamenitumia khabari ya kuwa nitoke kujiandaa na mapambano ya kuchomana mikuki na niwe tayari kwa vita vya upanga! Akina mama waombolezaji wawalilie.
Nilikuwa na ningali sihofishwi na vita wala kutishika na kupigwa. Nina yakini kwa Mola Wangu Mlezi na sina shaka na dini yangu”.

  • 1. Mdai: Ni mmoja katika watatu: wanaume wawili na mwanamke, ambao wametajwa katika kisa cha ngamia. (Man da'a waila madha ujiiba!? - Yaani ni kama kusema; Wadharauni watu walioitwa na mwitaji huyu! na liangalieni suala hili waliloitika wito kwa ajili yake kuwa ni baya mno.