read

23. Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Kuhusu mgao wa riziki:

“Hivyo, kwa kweli amri yateremka kutoka mbinguni mpaka ardhini kama matone ya mvua na kuifikia kila nafsi kiwango ilichogawiwa, ikiwa ni zaidi au pungufu, kwa hiyo endapo mmoja wenu anapoona kwa nduguye wingi wa ahli au mali au binafsi hilo lisimkere, kwa kuwa Muislamu hatendi kitendo ambacho lau kitafichuka atainamisha macho yake (kuona haya) na ambacho watu wasio na mashiko watashawishika, yeye ni mfano wa mcheza kamari anayetumainia mchezo wake wa kwanza utamhakikishia kipato na yakuwa utamfidia michezo ya nyuma aliyopata hasara.

Ni sawa na Mwislamu asiye na hiyana, anatazamia kwa Mungu mojawapo ya mazuri mawili: Ima wito kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na yaliyo kwa Mungu ni bora kwake. Au riziki ya Mungu, tayari ana watoto na mali, pia atakuwa na dini yake na hishma yake.

Na kweli mali na watoto ni matunda ya dunia tu, na matendo mema ni matunda ya akhera. Na Mungu (s.w.t) huenda akayakusanya mawili hayo kwa baadhi ya kaumu ya watu.

Jihadharini na yale Mungu Aliyo wahadharisheni, na mwogopeni kwa kiasi kwamba haitohitajika kuomba msamaha. Na fanyeni (wema) bila ya kutaka kujionesha au kusikika, kwa kuwa atendaye kwa ajili ya mwingine ambaye si Mungu, Mungu atamuwakilisha kwa yule aliyetenda kwa ajili yake.

Tunamuomba Mungu (s.w.t) mafikio ya mashahidi na tuishi maisha ya walio na maisha ya furaha, na kuwa pamoja na manabii.

Oh ninyi watu! mtu hawezi kujitosha - japo awe na mali - bila ya jamaa wa ukoo wake, na ulinzi wao juu yake kwa mikono yao na ndimi zao. Nao ni watu muhimu sana kwa uangalizi nyuma yake, nao ni kiunganishi mno cha mfarakano na ndugu zake, ni wenye huruma mno kwake anapokumbwa na shida. Utajo mwema Mungu amjaaliao mtu miongoni mwa watu ni bora kwake kuliko mali ambayo atawarithisha watu wengine”.

Utajo mwema kwa haki: Nao kwa ndugu ni bora na ni laiki yake:

Na miongoni mwa sehemu ya khutba hii: “Ala! Mtu asiache kusaidia haja aionayo kwa ndugu wa karibu, awaonapo katika shida azitatue, kwa kile ambacho hakitomzidishia au kumsaidia chochote akiacha, na wala hakitompunguzia chochote endapo atakitumia.

Na ambaye anauzuia mkono wake kuwasaidia ndugu zake wa karibu, ukweli ni kwamba unazuilika kutoka kwake kuwaendea wao mkono mmoja tu, na itazuilika kwake kutoka kwao mikono mingi. Mwenye tabia nzuri, mapenzi yake kwa ndugu yatadumu.

Maelezo: Amesema Sharif ar-Raadhiy; “Nasema Alghafiratu hapa ina maana ya kuzidi na uwingi, kutokana na usemi wao (Waarabu) kuhusu kundi la watu” Aljammau Alghafiru, yaani kundi kubwa la watu, na Aljam’u-Alghafiiru, ikiwa na maana hiyo hiyo. Na yaelezwa (If ’watun min Ahlin au mali) na Al’If ’watu; ni kitu bora, husema; Akaltu af ’wata ta’ami - nimekula chakula kilicho bora. Maana nzuri iliyoje aliyoikusudia (amani imfikie) kwa usemi wake mwenye kuuzuia mkono wake kwa kutowasaidia jamaa zake… mpaka mwisho wa usemi wake huo, kwa kweli mzuiaji kwa nduguye anazuia manufaa ya kheri ya mkono mmoja. Naye atakapohitaji nusura yao, na atakapodharurika na usaidizi wao, wao wata- jizuia kumnusuru, na watakuwa wazito kumpa sauti, kwa hiyo itakuwa umezuilika msaada wa mikono mingi, na kusimama nyayo nyingi.