read

24. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Katika kuhimiza kuwapiga vita Khawarij:

“Naapa kwa umri wangu siko legelege wala dhaifu katika kupigana na mwenye kuhalifu ukweli na kuyumbayumba ndani ya upotovu. Hivyo basi waja wa Mungu mcheni Mungu kimbilieni kwa Mungu kutoka kwa Mungu.1

Nendeni katika njia ya wazi aliyokufanyieni. Tekelezeni yale aliyowaambatanisha nayo. Kwa kuwa Ali ni mwenye kuchukua dhamana ya kufuzu kwenu hapo baadaye endapo hamtatunukiwa hivi punde.

  • 1. Kimbieni kutoka kwa Mungu kwenda kwa Mungu: Yaani, kimbieni kuielekea rehema ya Mungu kutoka adhabu yake.