read

26. Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Katika kuwalaumu waliomfanyia bai’a kwa sharti:

“Kwa kweli Mungu (s.w.t) alimtuma Muhammad (s.a.w.w) akiwa muonyaji kwa walimwengu na mwaminifu wa uteremsho (Qur’ani) na ninyi Waarabu mkiwa wafuasi wa dini ovu mno, na mkiwa mukiishi katika nchi yenye maisha magumu mno, kwenye mawe ya kwaruzayo na nyoka wenye sumu, mlikuwa mkinywa maji machafu sana na mnakula chakula cha ovyoovyo, mlikuwa mkimwaga damu zenu, mnakata mawasiliano na jamaa zenu. Sanamu zimesimamishwa mbele yenu, na dhambi zimekuambateni.”

Na sehemu nyingine ya khutba hii:

“Niliangalia na kuona sina msaidizi isipokuwa watu wa nyumba yangu, hivyo nilijiepusha kuwatumbukiza kwenye mauti, nilifumba macho yakiwa na chembe ya vumbi,1 na nilikunywa hali ya kwamba kooni kuna kilichokwama,2 na nilivuta subira katika kuvuta pumzi, na kwa uchungu mno kuliko ladha ya shubiri.”

Na sehemu ya khutba hii:

“Hakufanya baia3 hivyo basi haukufanikiwa mkono wa muuzaji na kutwezwa uaminifu wa mnunuzi,4 hivyo basi kuweni tayari kwa vita na mtayarishe zana zake, mwale wake umepanda na mwanga wake umepaa na mjiambatanishe na subira, kwa kuwa subira yaita kuelekea ushindi”.

  • 1. Na shajaa ni kitu kilichonasa kooni uwe mfupa wa samaki au mfano anaupiga Amirul Muuminina hali ya mambo ilivyomuiya ngumu mfano wa afumbuaye macho yake yakiwa yamejaa uchafu.
  • 2. Na amezaye sawa iwe maji au mfano wake akiwa na kilichomkwama kooni hiyo ndiyo hali iliyo mkabili Ali bin Abi Talib zama za ukhalifa wake.
  • 3. Asiyefanya bai’a hapa ni Amr bin Al-Aas mpaka alipoweka sharti apewe thamani ya baia yake. Amru bin Al-Aas alimwambia Muawiyah kuwa atamfanyia bai'a endapo atakubali kumpa uliwali wa Misri endapo mambo yatamnyookea.
  • 4. Mkono wa muuzaji ni Muawiyah bin Abii Sufiani, na ulitwezwa uaminifu wa mnunuzi!
    (yaani Amru bin al’Aas).