read

29. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Katika kuwalaumu wafanyao visingizio

“Enyi watu (mlio kama wale ambao) miili yao iko pamoja, wenye kutofautiana matakwa yao, maneno yenu yalainisha mawe magumu kabisa, na vitendo vyenu vyawatumainisha kwenu maadui! Kwenye vikao mwasema hili na lile, vita vikija mwasema tokomea mbali.

Wito wa mwenye kuwaiteni haupewi sikio wala moyo wa mwenye kuwachukulieni kwa nguvu hauwi na utulivu. Nyudhuru zisizo na maana. Mliniomba kurefusha muda, ni ulipaji wa mwenye deni msogeza muda, dhaifu hawezi kuizuia dhulma, na haki haipatikani ila kwa juhudi. Ni nyumba gani mtailinda baada ya nyumba yenu hii! Na kiongozi (imam) gani baada yangu mtaweza kupigana pamoja naye?

Wallahi aliyedanganyika ni yule mliyemdanganya, na mwenye kufaulu nanyi atakuwa amefaulu - Wallahi - na mshale usiofanikisha.1 Na mwenye kutupa na ninyi atakuwa ametupa kwa mshale uliovunjika maingiliyo ya kamba, Wallahi nimekuwa sisadiki kauli yenu, na wala situ- mainii nusra yenu, wala simkamii adui kwa kuwatumainia ninyi. Mmekuwaje? Dawa yenu nini? Nini tiba yenu? Hao watu ni wanamume kama ninyi. Ni kauli tupu bila ya ilmu, na mghafiliko bila ya kujiepusha, na tamaa katika ambalo si haki!?”

  • 1. Mwenye kufanikiwa na ninyi na mkawa hisa yake, atakuwa amefanikiwa na mshale usiofaa, nao ni mshale wa ramli usiokuwa na hadhi.