read

31. Na Miongoni Mwa Semi Zake (A.S)

Kwa ibni Abbas:

Alipomtuma kwa Zubairi akimtaka arejee kwenye utii wake kabla ya vita vya Jamal:

“Usikutane na Talha, kwa kuwa wewe endapo utakutana naye utamkuta yuko kama ng’ombe maksai amezipindisha pembe zake, anayaparamia magumu huku akisema: ‘Ni mepesi hayo,’ lakini kutana na Zubair, kwa kuwa yeye ana tabia laini, na umwambie: ‘Mtoto wa mjomba wako anasema: Ulinitambua toka Hijazi,1 na hunitambui Iraq, ni jambo gani limebadilisha yaliokudhihirikia!”

Maelezo: Amesema Ar-Radhiy (r.a.): Yeye (a.s) ni wa kwanza ambaye limesikika neno hili kutoka kwake, nakusudia: (Famaa ada mimmaa badaa) - nini kimemtoa mbali na lililomdhirihikia.

  • 1. Arifahu bil-Hijazi: Alimtii huko kwa kuwa alimfanyia bai’ya, na akaacha kumtambua huko Iraqi kwa kuwa alitoka dhidi yake na alikusanya watu ili kumpiga vita.