read

35. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Baada ya hukumu (tah’kiim):

“Shukrani ni za Mwenyezi Mungu japo zama zilete misiba mizito na tukio zito na kubwa.1
Na ninashuhudia kuwa hapana mungu isipokuwa Allah Mungu Mmoja peke Yake hana mshirika, hayuko mungu mwingine pamoja na Yeye, na kuwa Muhammad (s.a.w.w) ni mja Wake na mjumbe Wake.

Ama ba’ad, kwa kweli kumuasi mtoa nasaha mwenye huruma alie mjuzi mwenye uzoefu kunarithisha hasara, na matokeo ya majuto. Nami nilikuwa nimewaamrisheni amri yangu kuhusiana na hukumu hii,2 na nilikuwa mnyofu kwenu, kwa kuwapa rai yangu iliyohifadhiwa, lau ingetiiwa amri ya Qasiir!3

Mlinikatalia ukataaji wa wapinzani wakakamavu, na waasi wasio watiifu, mpaka mtoaji wa nasaha akaishakia nasaha yake4 na kijiwe (kigumu kama cha kiberiti) kilishindwa kutoa cheche zake,5 hivyo nikawa mimi na nyinyi ni kama alivyosema yule mshairi Hawaazin.6

Nilikuamrisheni amri yangu huko Mun’arajil-Liwa
Nasaha haikubainika isipokuwa baadae asubuhi ya kesho yake”.

  • 1. Makusudio ya tukio kubwa hapa ni tukio la mahakimu wawili.
  • 2. Hukumu hii hapa mradi wake ni hukumu ya mahakimu wawili: Amr bin Al’Aas na Abi Musa Al’Ash’ariy, na hii ilikuwa baada ya vita kusita kati ya Amirul’Mu’minina (Ali bin Abi Talib) na Muawiyah bin Abii Sufian katika vita vya Sifiin mwaka wa 37 A.H. Kwani jeshi la Muawiyah lilipoona limelemewa katika mapambano, Muawiyah alifanya udan- ganyifu kwa kuiangika misahafu (Qur’ani) juu ya mikuki akiomba ifanywe hukumu kwa mujibu wa Kitabu cha Mungu. Na vita vilikwishaangamiza watu wengi wa pande zote mbili, kwa hiyo wasomaji wa Qur’ani (al-Qurau) wakadanganyika, na kundi la watu likawafuata kutoka jeshi la Ali (a.s) wakasema: “Tumeitwa kwa Kitabu cha Mungu na sisi tunastahiki zaidi kukiitika.” Amirul’Mu’minina (a.s) akawaambia: “Kwa kweli hilo ni neno la haki linalokusudiwa batili, kwa kweli wao hawakuiinua ili waitekeleze hukumu yake, wao wanaijua wala hawafanyi kwa muujibu wake, hiyo ni hadaa, unyonge na hila, niazi- meni mikono yenu na fuvu zenu kwa saa moja, haki imefikia makatio yake, hakuna kilicho baki ila ukatwe mwisho wa waliodhulumu.”
    Wakaenda kinyume na wakatofautiana, vita vikaisha, na watu wakaongea kuhusu suluhu na tah’kiimu ya watu wawili wahukumu kwa yaliyo ndani ya Kitabu cha Mungu. Kwa hiyo Muawiyah alimteua Amr bin Al-Aas, na watu wa Amirul’Mu’minina wakamchagua Abu Musa Al’Ash’ariy, Amirul’Mu’minina hakuridhika na uteuzi huu, na badala yake alimch- agua Abdullah bin Abbas, wao hawakuridhika. Kisha alimchaguwa Malik Al’Ash’tar an- Nakh’i lakini hawakutii, akaafikiana nao uchaguzi wa Abu Musa Al’Ash’ariy akiwa amekirihishwa, baada ya kuwa alitaka udhuru katika kuwanasihi hawakutii, akawaacha; yaani alifanya ikhlas rai yake kuhusiana na suala la hukumu kwanza na mwisho, kisha suala la hukumu liliishia Abu Musa kufanyiwa hadaa na Amri bin Al’Aas, hadaa ambayo ilim- fanya Abu Musa amuengue Amirul’Mu’minina. Hilo likasababisha kudhoofu kwa Amirul’Mu’minina na sahiba zake.
  • 3. Yeye alikuwa mtwana wa Judhaima aliyekuwa maarufu kwa jina la Al’Abrash, alikuwa mwerevu. Alitoa ushauri kwa Bwana wake Judhaima kuwa asimwamini Zibaau Malikia wa Al-Jazira, akafanya kinyume na nasaha zake, na akamwendea ikiwa ni jibu la kutaka amuoe, yule malikia akamuua. Hapo ndipo Qasiir akasema: “Amri ya Qasiir haiti- iwi” tokea hapo ukawa mfano upigwao.
  • 4. Mpaka mtoa nasaha akaishakia nasaha yake (mtoa nasaha hapa yu ajikusudia yeye mwenyewe), kwa kuwa wao walikula njama kwenda kinyume na nasaha yake mpaka akaingiwa na shaka na nasaha yake na akadhania labda nasaha haifai, na labda sahihi ni lile walilokubaliana! Na hiyo ni sera ya mwanadamu endapo upinzani utakithiri dhidi ya yaliyo sahihi, mkweli hujituhumu binafsi.
  • 5. Kijiwe kilishindwa kutoa cheche zake: Yaani yeye baada ya hivyo haoni kuwa na rai iliyo sahihi kutokana na kukithiri kwa upinzani wao aliokutana nao, hali huwa hivyo kwa kila mtoa shauri mnasihi, akituhumiwa uoni wake hufifia na rai yake huharibika.
  • 6. Akhu Hawaazin: Yeye ni Duraid bin As-Simmah. Na Muna’ariju’liwa: Ni jina la mahali, na asili ya Liwa: ni mchanga mpya baada ya mchanga.