read

36. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Katika kuwahofisha watu wa An-Nah’rawan:1
Mimi ni mwonyaji kwenu, nakutahadharisheni msije kuwa waliotupwa chini wafu katika mto huu, na ardhi tulivu ya chini bila ya ubainifu wowote kutoka kwa Mola wenu Mlezi, wala hoja ya nguvu mliyonayo, mmekuwa katika myumbo na kudra imewatieni kamba.

Na nilikuwa nimewakatazeni hukumu hii - maamuzi mliyoyafanya - mkanikatalia ukataaji wa wapinzani wanaotupilia mbali, kiasi cha kunifanya niichukue rai yangu na kuitia kwenye utashi (potovu) wa nafsi zenu, na hali ninyi mkiwa wapumbavu wa akili - hamna baba - Mungu awaangamize! katika kuwakatazeni hukumu ile, sijawatakieni madhara yeyote.

  • 1. An-Nah’rawani: Ni jina la sehemu chini ya mto kati ya Al’Khafiqu na Tarafa’u, ulio karibu na mji wa Kufa upande wa jangwa la Haruurau. Na huitwa eneo la juu ya mto huo Taamir. Na ambao walikuwa wametoka dhidi ya utii wa Amirul’Mu’minina na wakamkosoa kuhusu tah’kiim na wakatangua Ba’ia yake, na walidhihirisha uadui wao kwake, na wakawa na vita dhidi yake, kwa hiyo wengi wao walijikusanya mahali hapo. Na wao wanaitwa ma-Haruriyah; kwa maelezo yaliyotangulia sababu ardhi ambayo walijiku- sanya ilikuwa inaitwa Haruura’u, na kiongozi wa kikundi hiki kipotovu Hur’qus bin Zahiir Assa’adiy, na laqabu yake ni Athudayyatu, dogesho la neno thadyu, Amirul’Mu’minina ali- watokea akiwawaidhi kuwataka wabatilishe usemi wao, na kuirejea Bai’a yao, kwa hiyo waliijibu nasaha hii kwa kuvurumisha mishale, na kuwauwa sahaba wake karrama llahu waj’hahu,Hapo ndipo aliamrisha wapigwe vita, kwa hiyo mapigano yalitanguliwa na onyo hili tunaloliona.