read

37. Na Miongoni Mwa Semi Zake (A.S)

Usemi huu waenda mwendo wa khutba:1

Na humo (a.s) anataja fadhaili zake aliisema baada ya tukio la An-Nah’rawan:

Nilitekeleza amri walipokuwa wameshindwa2…na nilijitokeza walipofichama, na nilitamka waliponyamaza, nilipita kwa nuru ya Mungu waliposimama. Nilikuwa wa sauti ya chini mno kati yao, na wajuu mno kwa kwenda mbele, na niliruka na hatamu zake, na nilikuwa wapekee kuikabili khatari iliyokuwa ikiepukwa. Na nilikuwa kama jabali halitikiswi na upepo mkali wala haimuondoi dhoruba. Yeyote hakuwa na la kuniaibisha nalo, wala msemaji hakuwa na la kunikebehi (yaani sikuwa na aibu mtu awezayo kuniaibisha nayo).3

Mnyonge kwangu ni mwenye hadhi mpaka nimrudishie haki yake, na mwenye nguvu kwangu ni dhaifu nitaichukuwa haki aliyodhulumu kutoka kwake.

Tumeyaridhia maamuzi yake Mungu,4 na tumesalimu amri yake Mungu. Je, mwaona mimi nimsemee uwongo Mjumbe wa Mungu (s.a.w.w)? Wallahi mimi ndimi wa kwanza kumsadiki, sitokuwa wa kwanza kumsemea uwongo. Niliangalia suala langu, na kuona utii wangu yapasa uitangulie ba’iah yangu, hali ikiwa ahadi yangu imekuwa mzigo shingoni mwangu.5

  • 1. Usemi huu Ar-Radhiy ameuleta kana kwamba ni kipande kimoja chenye lengo moja, wala sivyo, ni kipande hakikurubiani. Kila kipande miongoni mwavyo kina maana isiyokuwa kwenye kipande kingine. Ar-Radhiy (r.a) alikidondoa kutoka kwenye maneno ya Amirul’Muuminina (a.s) marefu yaliotawanyika, aliasema baada ya tukio la An- Nah’rawan, humo aliieleza hali yake tokea alipotawafu Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) mpaka mwisho wa wakati. Kwa hiyo Ar-Radhiy akavifanya alivyovidondoa miongoni mwavyo kimoja kimoja, na vimekuwa kwa msikilizaji kana kwamba kwavyo yu-alenga lengo moja. Nayo imo katika milango minne; wa kwanza: Kauli yake: “ fa qumtu bil’am- ri” mpaka kauli yake: “wastadarta burhanaha.” Na mlango wa pili tokea kauli yake: “Kal-jabali la tuhariquhu al-qawaswifu,” mpaka kauli yake: “hatta akhadhal-haqa minhu.” Na mlango wa tatu: tokea kauli yake: “radhwiina anillahi qadhwa’ahu.” Mpaka qauli yake: “fala akunu awwala man kadhaba alayhi.” Na mlango wa nne: yaliobakia.
  • 2. Yaani nilikataza munkari waliposhindwa sahaba wa Muhammad (s.a.w.w) kufanya hivyo. Anaielezea hali yake kipindi cha ukhalifa wa Uthman, na nafasi yake katika kuam- risha mema na kukataza munkari (mabaya) siku za matukio, yaani yeye alikataza munkari waliposhindwa kaumu.
  • 3. Na huu ni mlango wa pili anataja hali yake baada ya Ba’iah kuwa yeye aliutekeleza ukhalifa akiwa kama jabali….
  • 4. Kauli yake: (Radhwiinaa…) ni maneno aliyasema alipokuwa akikagua kaumu kwa makini katika askari wake kuwa wao wanamtuhumu katika anayowapa habari kutoka kwa Nabii kuhusu habari za mapambano na mambo ya ghaibu.
  • 5. Usemi wake“Niliangalia kuhusu suala langu”: Jumla hii ni kipande kutoka usemi wake kuhusu hali yake binafsi (ilivyokuwa) baada ya kutawafu Mtume wa Mungu (s.a.w.w.), alibainisha kuwa aliamriwa awe mpole katika kuitaka haki yake, akaitii amri katika ba’ia ya Abu Bakar, Umar na Uthman kwa kulinyamazia hilo.