read

38. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Akielezea maana ya shub’hah (kushabihiana):

Shub’ha imeitwa hivyo kwa sababu inashabihiana na ukweli, ama wapenzi wa Mungu, mwanga wao humo ni yakini, na dalili yao humo ni nji ya mwongozo. Ama maadui wa Mungu wito wao humo ni upotovu, na dalili yao ni upofu. Hatoepuka umauti mwenye kuuogopa.1

  • 1. Usemi wake: “hatoepuka umauti…” hauna uwiano na usemi wa kabla yake, usemi huo ni kipande cha maneno mengine amekiambatanisha na huu kama alivyokusanya milango iliyotangulia.