read

39. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Kuwalaumu wanaobaki bila ya kwenda vitani:

Nimekumbwa na balaa la wasiotii nitoapo amri, wala hawaitikii nikiita. Hamna baba! Mnangoja nini kwa kumnusuru Mola wenu?

Hapana dini iwezayo kuwakusanya, wala hisia ya aibu kuwaghadhibisheni! Nasimama kati yenu nikiomba nusra, na nakuiteni nikiomba usaidizi, wala hamnisikilizi usemi wowote, wala kunitii amri, mpaka yafichuke matokeo mabaya! Kisasi hakilipwi pamoja na ninyi, wala lengo halifikiwi pamoja na ninyi. Niliwaita ili muwanusuru ndugu zenu mkakoroma mkoromo wa ngamia aliyepatwa na maradhi … na mkawa wazito kama uzito wa ngamia aliyekonda mwenye kujeruhiwa kisha nikajiwa na kikosi kutoka kwenu, dhaifu kikinepanepa; (Kana kwamba wanasukumwa kwenye mauti nao wanaona; 8:6)

Maelezo: Ar-Radhiy (r.a) amesema: Usemi wake (a.s): (mutadhai-bun) yaani yenye kuyumbayumba; kutokana na kauli yao: (tad- ha’abati riihu) yaani upepo umeyumbayumba, uvumapo ukiyumba, kutokana nalo hilo mbwa mwitu amepewa jina hilo kwa sababu ya kuyumbayumba mwendo wake.