read

40. Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Kuhusu Khawariji alipoisikia kauli yao: “Hakuna hukumu ila ya Allah”

Na neno ni la kweli lakini linakusudiwa batili! Naam ni kweli kuwa hapana hukumu ila ni ya Mungu, lakini hao wanasema: Hapana uamiri ila wa Mungu. Na kwa kweli watu hapana budi wawe na mtawala mwema au muovu,1 mu'umin atenda (mema) katika utawala wake,2 na kafiri anastarehe humo, na Mungu aufikisha humo muda,3 na hukusanywa (kwa utawala wake) kodi, pamoja na yeye hupigwa vita adui, pamoja naye njia zabakia na amani, pamoja naye huchukuliwa (haki zilizodhulumiwa) kutoka kwa mwenye nguvu kwa ajili ya mnyonge; Ili mwema apumzike na ili muovu apumzishwe

Na katika riwaya nyigine ni kuwa yeye (a.s) aliposikia hukumu yao akasema:

“Hukumu ya Mungu naingoja iwe kwenu.”

Na akasema: “Ama utawala mwema mchamungu humo hutenda mema, ama utawala muovu hustarehe humo mwenye mashaka (shaqiy); mpaka muda wake ukatike na mauti yake imkute”.

  • 1. Ni dalili ya kuwa dhana yao batili kuwa hapana utawala ila ni wa Mungu ni: Hali ya dhahiri yaamua kuwa watu hapana budi wawe na mtawala mwema au muovu; ili mambo yao yanyooke. Na utawala wa muovu haumzuii mu'umini kutenda matendo yake (ya kiimani) ili kuilinda dini yake na dunia yake, na humo kafiri anastarehe mpaka ajali imchukue, na Mungu ayafikishe mambo muda wake uliopangiwa kulingana na nidhamu ya kimaumbile. Na maslahi zilizotajwa ziendelee. Na yawezekana ikawa kusudio la mu'umi- ni hapa ni amiri mwema na mradi wa kafiri ni mtawala muovu, kama ijulishavyo riwaya nyingine. Na kauli yake
  • 2. Mu'min anafanya humo, yaani si kizuizi kwa mu'min kufanya: kwa sababu anaweza kuswali, akafunga, na kutoa sadaka japo kuwa mtawala ni muovu. Na kafiri akastarehe humo: yaani akastarehe na muda wake.
  • 3. Na Mungu anaufikisha muda humo; kwa sababu utawala wa muovu ni kama utawala wa mwema, kwamba muda uliowekwa mwanadamu utaisha humo.