read

41. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Na miongoni mwa Khutba yake (a.s) - Ameitaja ibn Talha katika kitabu Matalibus-Su’ul, Jz. 1, uk. 170

Kuhusu utekelezaji na ukweli:

“Enyi watu! Kwa kweli kutekeleza ahadi ni pacha wa ukweli,1 siijui kinga yenye kuhifadhi mno kuliko hiyo (kwa shambulio la dhambi) wala hafanyi uhaini mwenye kujua marejeo yalivyo.2

Kwa kweli tumeingia katika wakati ambao walio wengi miongoni mwa watu wake wameufanya uhaini kuwa ni uwerevu, na wajinga wamewanasibisha watu kama hao kuwa huo ni ujanja mzuri. Wamekuwaje (watu hawa)! Mungu awaangamize!

Na mwenye uzoefu na uelewa wa mambo ya maisha anao udhuru wa kumzuia asitekeleze amri na makatazo yake Mungu, lakini hautilii maanani ingawaje anao uwezo, akawa yu ajua hila, na pembeni mwake kuna kizuizi miongoni mwa amri ya Mungu na katazo lake lakini anaacha baada ya kuwa alikuwa na uwezo wa kutenda hayo, na huitumia fursa hiyo asiye na kizuizi cha kidini.

  • 1. Kutekeleza ahadi ni pacha wa ukweli: Kwa kuwa utekelezaji ahadi hakika yake ni ukweli; na sidqu ambao ndio ukweli, kwani ukweli na utekelezaji ahadi kuwa kwao ni nira, mmoja hamtangulii mwenzake katika kuwa wala daraja.
  • 2. Yaani mwenye kuijua akhera na ajua kuwa marejeo yake ni kwa Mungu naye ni Mwepesi wa kuhasibu hawezi kuhaini; kwa sababu uhaini unaharibu imani.