read

44. Na Miongoni Mwa Semi Zake (A.S)

Tabariy ameyataja ndani ya tarehe yake, Jz.6, uk. 65, na Ath- Thaqafiy ndani ya Al-Gharatu, na Al-Baladhuriy ndani ya Ansabul’ash’rafi, uk. 411. Masqalat bin Hubairat Ash-Shaibaniy alipokimbilia kwa Muawiyah, na alikuwa amekwishawanunua mateka wa Bani Naajiyata kutoka kwa mfanyikazi wa Amirul’Mu’minina (a.s) na kuwaacha huru, na alipomdai mali ya malipo alimfanyia udanganyifu na akakimbilia Sham.1

“Mungu amuweke mbali na rehema Masqalah! Amefanya kitendo cha mabwana, na amekimbia ukimbiaji wa kitwana, kwa hiyo msifiaji wake hakutamka kwani amemnyamazisha, na wala mfanya wasifu wake hajaeleza kitu bali amemkemea, lau angebaki tungechukua kutoka kwake kile ambacho ni chepesi kwake kukilipa, na tungengoja kuzidi mali yake.”

  • 1. Al-Khuraitu bin Rashid An-Najiy alikuwa mmoja katika Bani Naajiyata na alikuwa pamoja na Amirul’Mu’minina katika vita vya Siffin, baada ya vita ya Siffin aliitangua ahadi yake, na alimlaumu katika suala la tah’kiim, na alitoka huku akiwaharibu watu na kuwashawishi waende kinyume (na Amirul’Mu’minina), Amirul’Mu’minina akamtumia kikosi akiwemo Ma’aqilu bin Qays Ar-Rayahiy ili kumpiga vita yeye na waliojiunga pamwe na yeye, kikosi kilimdiriki akiwa Saiful’bah’ri huko Uajemi, na baada ya kuitwa atubie na kukataa kukubali aliandamwa na kuuliwa, na waliuliwa pamwe na yeye wengi katika watu wa kaumu yake, na walichukuliwa mateka waliokutwa ndani ya msafara wao waume kwa wake na watoto, na walikuwa mateka mia tano. Na Ma’aqilu aliporudi na mateka, alimpitia Masqalah bin Hubayrah As-Shiibaniy, na alikuwa mtendaji mtumishi wa Ali katika Ardashiiri khurh. Wanawake na watoto walimlilia, na wanaume walipiga mayowe wakimsihi waachiwe, kwa hiyo akawanunua kutoka kwa Ma’aqil kwa dirham mia tano elfu, kisha alikataa kulipa kile kiwango, na madai ya malipo ya ile haki yalipo mtopea alikimbilia kwa Muawiyah chini ya sitara ya usiku.