read

45. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Nayo ni miongoni mwa khutba ndefu alihutubia siku ya Eid al’Fitri, akiilaumu humo dunia:

“Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye rehema Yake haikatishi tamaa, wala hakuna anayeepukana na neema Yake, wala haukatishi tamaa msamaha wake, wala hafanyiwi kiburi kwenye ibada yake, ambaye kwake haikosekani rehema, wala haachi kuwa na neema.

Dunia ni nyumba iliyokadiriwa kuisha, na watu wake kutoweka humo, nayo ni tamu, ya (rangi) kijani.1 Na kwa kweli imemharakia mwenye kuitaka, na imejiangika moyoni mwa mwenye kuitamani. Ondokeni humo mkiwa na masurufu yaliyo bora,2 wala msiombe humo zaidi ya linalotosha,3 Wala msiombe kutoka humo zaidi ya mlo.

  • 1. Ni tamu na rangi kijani: Maneno ya mfano, yaani kuifananisha dunia na kinachozoeleka na yapendwayo na nyoyo na kuburudika macho. Imechukuliwa kutoka kauli yake (s.a.w.w.): Kwa hakika dunia ni tamu rangi ya kijani, na kwa hakika Mungu amekuwekeni humo angalieni jinsi mtakavyotenda.
  • 2. Yaani muwe na maandalizi yaliyo bora kwa mazuri mliyonayo, nayo ni tabia njema na matendo mema.
  • 3. Yaani msiombe zaidi ya riziki inayokutosheni.