read

47. Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Katika kuuelezea mji wa al-Kufa

“Ewe al-Kufa! nakuona kana kwamba unawambwa mfano wa ngozi iliyotiwa rangi (iliyodibaghiwa) katika soko la Ukaadhu1 unapambana na shida, na wakumbana na misukosuko, nami najua fika kuwa mjeuri anapo kukusudia kwa uovu Mungu humshughulisha na balaa au humtupia muuwaji.”

  • 1. Ukaadhu: Ni jina la soko la Waarabu hapo kale upande wa Makah lilikuwa jangwani katika eneo kati ya Nakh’latu na Ta’aifu, walikuwa wakijikusanya hapo kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa Dhulqaadah - mwezi wa kumi na moja - ili kujifaharisha - kila mmoja na alichonacho miongoni mwa ubora na uhodari wa ushairi, hivyo: ta’aqadhu ni kujifaharisha, soko lilichukua jina la yaliyokuwa yakifanyika hapo. Walikuwa wanabaki hapo mwezi huku wakifanya biashara na kufanya nishadi tenzi za mashairi. Abu Dhuaybi amesema:
    (Kuba zikijengwa hapo Ukadhu, biashara huanza na maelfu hujikusanya. Ulipokuja Uislamu ulibomoa hayo, na mara nyingi ilikuwa yauzwa ngozi iliyodibaghiwa. likanasibishwa jina hilo. wal adiimu: ni ngozi iliyodibaghiwa, na jam’ul adiimi ni udumu, na huenda ikafanywa alaa adimati kama wasemevyo: Raghiifu wa arghifa, (watumaddina maddal-adimi) ni istiara kwa sababu ya kukabiliwa na maafa ya hapa na hapa.