read

48. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Alipokuwa akienda Sham:

“Shukrani ni zake Mungu kila usiku uingiapo na giza linapokithiri, na shukrani ni za Mungu kila nyota inapojitokeza na kila inapozama. (Mungu amesema: Na shari ya giza la usiku liingiapo; 113:3). Na himidi ni ya Mungu hakosi kuneemesha, wala halipwi fadhila.

Kwa kweli nimekwisha tuma kikosi cha mbele cha jeshi, na nimewaamuru wabakie kwenye ukingo wa mto wa Dajlah (Tigris), mpaka wajiwe na amri yangu, nimeonelea niyavuke maji haya mpaka makazi madogo ya watu miongoni mwenu wanaokaa ukingo wa mto wa Dajlah (Tigris), ili niwasimamishe pamwe na ninyi mumwelekee adui yenu, na niwafanye wawe nyongeza ya nguvu kwenu.”

Sharifu Ar-Radhiy anasema: ‘Anakusudia (a.s) kwa neno Miltaat hapa, upande aliowaamuru wabakie; nao ni ukingo wa mto wa Furaat, nalo latumika pia kwa ukingo wa bahari. Na asili ya neno ni ardhi iliyo tambarare. Na yu akusudia kwa neno nut’fah: maji ya Furaati, na hiyo ni miongoni mwa ibara ya aina yake na ya ajabu.’