read

49. Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Kuhusu sifa ya Rububiya umola ulezi na ilimu ya Kiungu:

Mwenye kustahiki sifa ni Allah (swt) ambaye ameficha mambo yaliyofichikana, na yamejulishwa na dalili zilizo dhahiri, na amezuilika na jicho lenye kuona;1 hivyo basi hapana jicho la asiyemuona linalomkanusha2 wala moyo wa aliyemthibitisha unaomuona.3 Ametangulia katika kuwa juu hapana kitu kipo juu zaidi yake, na amesogea kwa ukaribu hapana kitu kilicho karibu mno kuliko Yeye.4 Hivyo basi si kuwa juu mno kwake kumemuweka mbali na kitu katika viumbe Vyake, wala si ukaribu wake umewafanya viumbe wawe sawa naye katika mahali.5

Hajazijulisha akili mipaka ya sifa Zake, wala hakuzizuia kiasi cha kuwa mbali na wajibu wa kumtambua kwake, hivyo basi Yeye ndiye ambaye alama za kuwepo zamshuhudia, kwa kukiri moyo wa mwenye kupinga,6 Mungu yu aepuekana na wayasemayo wamshabihishao na wanaompinga, yu juu juu juu kabisa!”

  • 1. Amezuilika na jicho lenye kuona (Anasema: Kuwa Yeye (swt) haonekani kwa uoni wa jicho, pamoja na hali hiyo haiwezekani kwa asiyemuona kwa jicho lake amkanushe (kuwa hayupo); kwa sababu kila kitu ni dalili ya kuwako kwake, si hivyo tu bali Yeye mwenyewe (swt) kuweko kwake ni dalili tosha.
  • 2. Hapana jicho la asiyemuona linalomkanusha (yaani asiyemuona hamkanushi kwa kutegemea kutomuona kwake; kwa sababu ya kudhihiri dalili nyingi kumuhusu.
  • 3. Wala hapana moyo wa aliyemthibitisha (kuwepo kwake) unaomuona (Yaani: hapana njia kwa aliethibitisha kuwepo Kwake ilimu yake imtambuwe kwa kuzizunguka hali Zake zote na maalumati Yake na matengenezo Yake, au amekusudia kuwa hakika ya dhati Yake haijulikani; kama walivyosema jamaa wahakiki. Yaani hapana njia kwa aliyemthibitisha kuwepo Kwake, ilimu yake imzunguke na kumjuwa hali Zake zote na maalumati Yake na matengenezo Yake, au amekusudia kuwa yeye haujulikani ukweli wa dhati yake; kama walivyosema kaumu ya watu miongoni mwa wahakiki. Na maneno haya yameelezwa kwa njia nyingine, wamesema kuihusu hutuba hii: (Hapana moyo wa asiyemuona unaomkanusha, wala jicho la aliyemthibitisha linalomuona), Nayo ndiyo muwafaka zaidi.
  • 4. Amekuwa juu kuliko kila kitu kwa dhati Yake na ukamilifu Wake na utukufu Wake, na amekuwa karibu na kila kitu kwa ilimu Yake na irada Yake na kuvizunguka kwake na kuvi- tilia manani kwake, kwa hiyo hapana kitu isipokuwa Yeye yu pamoja nacho na hapana kitu kimbali naye.
  • 5. Kuwa juu Kwake hakujamuweka mbali (Kuwa juu kwake hakulazimiani na mahali kwa kuwa mbali na vitu vyenye miili, wala ukaribu wake haulazimu kuwa sawa navyo kwa kuhitajia mahali na upande, kwa sababu kuwa juu Kwake na kukaribia Kwake sio katika sura ya sehemu na mahali.
  • 6. Kwa kweli moyo wa mpingaji japo akanushe, ukanushaji wake sio kingine ila ni athari ya sababu za nje ya maumbile yake, na kudhihiri alama za kuwepo katika kumjulisha, moyo wa mpinzani hauwi na nguvu kuizuia taathira, kwa hiyo yeye haepuki kukiri kwa ukweli hasa, japo kujitokeze kukanusha katika maneno yake na baadhi ya matendo yake.