read

50. Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Miongono mwa maneno yake (a.s)- Hotuba hii Al’Barqii ameielzea katika kitabu “Al’Mahasin” katika
kitabu cha ‘Masabiihu dhulmi’.
Na at-Tawhidii ndani ya “Al’Basairu wa Dhakhairu” uk. 32. Na ibn
Waadhihu ndani ya “At-Tari’ikh”: Jz. 2, uk. 136. Na Al’Kaulayni ndani ya “Al’Kaafii” katika mlango wa Al’bid’au war’ra’ayu

Kuhusu chanzo cha fitna:

“Hakika chanzo cha kutokea fitina ni kuendekeza na kufuata matamanio, na hukumu huzushwa, humo Kitabu cha Mungu huendwa kinyume, kwa hilo watu wanasaidiana wao kwa wao1kinyume na dini ya Mungu. Lau batili ingekuwa tupu bila ya kuchanganyika na haki isingefichika kwa wenye kuitafuta; Na lau haki ingekuwa imeepukana na kuvikwa na batili, ndimi za wapinzani zingekatika.

Lakini huchukuliwa kutoka huku fumba2 na huku fumba na huchanganywa, hapo shetani huwashinda rafiki zake, wataokoka wale waliotunukiwa wema kutoka kwa Mungu hapo kabla.”

  • 1. Watu wanasaidiana. Anasema (a.s): Kwa kweli madhehebu za batili na rai mbovu ambazo kwazo watu wanakumbwa na fitna, asili yake ni kuifuata hawaa - matamanio ya nafsi, na kuzua hukumu ambazo hazikujulikana (na dini) zilizo kinyume na Kitabu, ushabiki na matamanio ya nafsi humchukua mtu kuwapenda watu wayasemayo hayo (ya bid’a), bila ya uthibitisho kutoka (dalili za) dini. Nguzo ya kutokea kwa mkanganyiko huu wote ni kule kuchanganyika kwa haki na batili katika maoni.
  • 2. Fumba: (fumba hapa ni tafsiri ya: yaani ujazo mmoja wa kicha cha majani yaliyochanganyika kati ya mabichi na makavu, Mungu (swt) amesema: “Na shika kicha cha majani mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho” (Surat Swad: 44). Anamaanisha (a.s) kuwa ikitendwa haki kama ilivyo haitoshabihiana na batili, iangaliwapo batili hujitokeza kana kwamba kuna sura ya haki kwa hiyo anakanganyikiwa, hiyo ndiyo fumba la haki na hiyo ni: fumba la batili. Na machimbuko ya matamanio ya kinafsi ndio chanzo cha kutokea kwa fitna, na hiyo ni kutokana na kuchanganyika kati ya haki na batili.