read

51. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Na miongoni mwa khutba zake (a.s) - Ameieleza hotuba hii ibn Muzahim ndani ya kitabu chake,‘Swifiin.’

Watu wa Muawiyah walipowazidi nguvu watu wake (a.s) kwa kuzingira njia ya maji na kuwaziwia wasiteke maji kutoka mto wa Furati huko Siffin:

“Wamekuombeni vita, basi bakieni katika madhila na kubaki nyuma kwa daraja, au zikozeni kiu panga kwa damu mtakoza kiu zenu kwa maji: Mauti hasa ni maisha ya kuburuzwa, na uhai hasa ni kufa ndani ya kutenzwa nguvu. Lo! kwa hakika Muawiyah ameongoza kikundi cha watu waasi na amewafichia kheri kiasi cha kuwa wamezifanya shingo zao ziwe shabahio la mauti.”