read

53. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Katika kuielezea siku ya kuchinja na hali ya mnyama atakiwaye kuchinjwa:

“Na miongoni mwa ukamilifu wa mnyama achinjwaye ni kunyooka na kuinuka masikio yake na usalama wa macho yake. Endapo masikio na macho yatakuwa salama, mnyama wa kuchinjwa atakuwa amekamilika na ametimia. Japo awe mweye kuvunjika pembe na yu auvuta mguu wake kwenda machinjioni”.1

Sayyid Ar-Radhiy amesema: Na mansaku hapa ni mahali pa kuchinjia.”

  • 1. Anakokota mguu wake akielekea kwenye machinjio: Maana yake ni kinaya cha aliyelemaa mguu (kiguru). Na katika sifa za mnyama wa kuchinjwa na aibu zake, kuna maelezo na tofauti nyingi ndani ya vitabu vya fiqhi.