Mateso Ya Watumwa

Tumekwisha ona Uislam ulichofanikiwa katika kupunguza ukali wa maumivu ya taabu ya watumwa na jinsi gani, kwa mara ya kwanza na mara ya mwisho katika historia, watumwa walivyopewa hadhi ya ubinadamu wakiwa na haki juu ya wamiliki wao. Sasa hebu tuangalie jinsi Wakristo walivyo watendea watumwa wao. Kabla ya kutoa maelezo, lazima niweke jambo moja wazi. Maelezo haya ni ya kuhusu taabu za watumwa katika kipindi cha karne tano zilizopita ambapo, kama ilivyoelezwa mapema, Wakristo walianza biashara ya watumwa ya huko nyuma katika kiwango kisichoeleweka. Kama nilivyoonyesha kwenye sura iliyo pita, Waarabu pia waliwapa Wakristo msaada katika jambo hili kwa hiyari yao katika kipindi cha robo ya mwisho ya karne ya kumi na nane.

Kwa kuwa maelezo mengi mno ya nchi za Ulaya kuhusu biashara ya utumwa katika bara la Afrika, huanza kwenye kipindi hiki, kwa hiyo yapo maelezo mengi yaliyo wazi kabisa kuhusu yale yaliyoonekana na watu huko. Hivyo, Wakristo lazima wabebe uzito wa kuhusika na machukizo haya kwa kiwango kikubwa. Wakristo walikuwa wanawapa mateso haya kwa kipindi cha karne nne ikilinganishwa na karne moja ambayo ndicho kipindi ambacho Waarabu waliungana nao katika kuwashawishi ingawaje walihiyari kufanya hivyo.

Waathirika hao walikuwa Waafrika masikini wasiokuwa na ulinzi, watu wewusi (manegro) wa pwani ya magharibi na Mashariki ya Afrika na pia waliotoka katikati ya bara hilo. Waafrika walifanywa kama mali inayohamishika tu na vitendea kazi au viliyo vibaya zaidiya hapo. Ilibidi wafanye kazi, au pengine walilazimishwa kufanyakazi katika masharti yaliyo magumu sana kwenye mashamba mapya yaliyomilikiwa na mabwana zao, mataifa yenye nguvu yaliyo ya Kikristo ya nchi za Magharibi, ambao walichukua na kuvimiliki visiwa vyote kuvuka bahari ya Atlantic na katika ulimwengu mpya na vile vile hata nyumbani nchini Ureno na Hispania na nchi za Ulaya ya kati ya Ufalme Mtakatifu wa Kirumi chini ya miliki ya mapapa wa Kanisa Katoliki.

Mateso ya biashara ya utumwa yalijitokeza zaidi wakati wa robo ya mwisho ya karne ya kumi na tisa. Popote pale uvamizi ulipofanyika kijijini, vifo na uharibifu vilifuatia (vilitokea). Watu wengi zaidi walikufa wakilinda nyumba na familia zao, au kutokana na matokeo ya njaa na magonjwa ambayo kwa kawaida yalitokea baada ya vurugu kama hizo kuzidi, basi watu wengi waliofanywa kuwa watumwa, achilia mbali na wale waliouzwa huko pwani.

Mtu anaweza kutetemeka anapofikiria njia mbaya sana na za kikatili mno zilizotumika kuwakamata wazalendo masikini wa Afrika, walitenganishwa na ndugu zao, walichukuliwa na kutendewa vibaya zaidi kuliko hayawani. Sasa tutatoa maelezo mafupi kutoka kwenye vitabu vyao wenyewe, vya waandishi wa nchi za magharibi ili tuonyesha jinsi gani watumwa walivyoteswa na mbinu zipi za kikatili zilizotumiwa na wawindaji wa watumwa. Mbinu zao wakati fulani zilitekelezwa kiholela, na ziliingiza hasara, kwa sababu walikuwa wezi, si wapiganaji. “Utendaji wao ulikuwa kuzunguuka vijiji kadhaa ambavyo waliviteua kuvivamia, walinyemelea kimya kimya wakati wa usiku. Kwa kawaida kijiji kilikuwa kimejengeka kwa vibanda vilivyojengwa kwa tope ya kawaida na kuezekwa kwa mianzi na majani ya mchikichi, vyote hivi vikiwa vinashika moto na kuungua kwa urahisi sana, kwa hiyo, wavamizi walichoma moto vibanda hivyo bila aibu wala haya, na mara nyingi wali- fanya hivyo wakati wa alfajiri.

Wakazi wa vibanda hivyo walipoamka kutokana na mngurumo wa moto unaowaka kwa ukali walijikuta hawana la kufanya isipokuwa kukim- bilia nje, ambako huko walizingirwa na kukamatwa. Yeyote miongoni mwao aliyejaribu kuleta upinzani, aliuawa, kwani wawindaji wa watumwa hawakuwa na huruma.

Wazee na wasiojiweza na watoto wachanga waliuawa hapo papo kwani hawakuwa na shida nao, na ni wale tu wanaume na wanawake wenye nguvu, na wavulana na wasichana, waliachwa hai, ili wapelekwe utumwani, huku nyuma wakiacha maiti tu na majivu ya nyumba zilizoungua, mahali ambapo hapo mwanzo palikuwepo familia zenye furaha na makazi yaliyokuwa yanashamiri. Hasara ilikuwa kubwa mno kuzidi hiyo zawadi. Lakini uharibifu, mkubwa mno ilikuwa kama alama ya utumwa wa watu weusi, tangu nyakati zake za mwanzo, hadi mwisho. Popote pale utumwa ulipotokeza hali iliyofuata, ni vifo, magonjwa na maangamizi.

Watu waliokamatwa kutoka katikati ya mikoa ya bara walikuwa na bahati mbaya kidogo, walilazimika kutembea kwa miguu yao hadi pwani – mwendo mrefu wa kuchosha na kutia huzuni wa maili nyingi na msitu mnene na jangwa baya. Walitembea bila kuwa na nguo za kutosha, bila ya kinga yoyote dhidi ya miba mikaliu na mawe yenye ncha chonge na yenye kukeketa. Ili kuwazuia watumwa wasitoroke, walivishwa kongwa shingoni, wale waliokuwa wasumbufu, mikono yao iliingizwa kwenye ubao unao kwaruza wenye matundu, visigino vya miguu yao ilifungwa kwa minyororo.

Misitari mirefu iliyojulikana kwa jina la watumwa, iliunganishwa kwa kamba, walisafiri mwendo, mrefu kwa taabu kuelekea kwenye hatima yao ya kutisha, kwani Waafrika wote walikuwa wakielewa kwamba wazun- gu walikuwa wanakula nyama ya watu weusi ambao waliwanunua kutoka kwenye boma. Wamiliki wao waliwaswaga mbele kwa mateso makali na bila kupumzika, bila kujali majeraha na mikwaruzo ya ngozi, waliishiwa na nguvu kwa sababu ya kuchapwa mijeledi mingi. Kama kuna yeyote aliyeelemewa na mateso hayo na akashindwa kabisa kuendelea mbele, alitupwa pembeni mwa njia, na kama kuna mmoja wao alizidiwa na maradhi, aliachwa afe au kwa kuhurumiwa zaidi aligongwa kichwa ili afe haraka.” 1

“…Kwenye hali ya hewa nzuri au mbaya, pamoja na magonjwa na vifo, na kwa maasi yote na kujiua wenyewe, kila mwaka meli zilileta maelfu ya watumwa Marekani na katika visiwa vya West Indies. Walikuja kwa meli za mataifa mengi: Ufaransa, Udachi, Ureno, na Danmark – lakini zaidi ya nusu waliletwa na meli za Kiingereza ambazo zilisafiri kutoka Bristol, London, au Liver pool. Kila mwaka, walifikishwa pwani katika hali ya kuugua au wazi- ma wa afya, wakiwa wamekubali matokeo ya maisha au kukata tamaa na daima milele hawakurudi tena walikozaliwa… Matumizi ya watumwa, kama ilivyo matumizi yake mabaya, kamwe hayabadiliki; yalifanana kote duniani na kutoka kipindi kimoja hadi kingine.

Huko Marekani na katika visiwa vya West-Indies, kama ilivyokuwa wakati wa Rumi ya kale, au Ugiriki au mwanzo wa historia isiyo dhahiri, utumwa uligawanywa kwenye aina mbili pana utumwa wa kutumika ndani ya nyumba na utumwa wa kutumika mashambani.” 2

Sasa ngoja tuoneshe nukuu zingine zaidi kutoka kwenye kitabu hicho hicho “Freedom from Fear or the Slave and his Emancipation” kilicho andikwa na O.A. Sherrard, kuonye- sha jinsi gani na kwa kiwango gani mataifa ya mwanzo kabisa ya Kikristo kutoka Magharibi yalivyowatesa kinya- ma mno bila ya huruma watu Weusi ambao hawakuwa na namna yoyte ya kujilinda. Pia msomaji ataona imani na fiki- ra zao duni kuhusu binadamu ambao walitofautiana nao kwa rangi na taifa.

“Tukiangalia historia kwa mapana yake, walipita katika hatua mbili: katika hatua ya kwanza uvumilivu mabegani mwao, kama Atlas mstahamilivu, utukufu wa mamlaka nyingi zilizostaarabika zilizokufa zamani; na hatua ya pili yenye kudhalilisha zaidi kuliko ya kwanza, walipoteza hata ile heshima ya uwakilishi, na kuanguka kwenye hali ya unyonge ambamo mchango wao ulikuwa kutumikia uroho wa watu binafsi.
Hali yao, hasa zaidi katika hatua ya pili, wangeweza kuiogopesha dhamiri mbaya ya dunia ya Kikristo kwa jina, lakini jambo la kushangaza ni kwamba waliiacha hivi hivi bila yenyewe kusisimka. Wazo la utumwa lilikolea sana hivyo kwamba hakuna mtu aliye hoji usahihi wake. Mataifa yote ama yalifumbia macho au yalifurahia jambo hilo.” 3

Watumwa wengi waliofanya kazi kwenye mashamba, kazi yao ilikuwa ngumu sana, kazi aliyopewa, kwa mawazo yake ilikuwa kazi ya kifundi; alitakiwa kulima zao ambalo lilikuwa geni kwake – kwa sehemu kubwa miwa katika visiwa vya West Indies, pamba na tumbaku huko Marekani na kwamba kazi yake ilikuwa mpya alistahamili mzigo mzito zaidi kuliko mwenzake huko Ugiriki au Rumi au miongoni mwa watwa na wajakazi wa Ulaya… Kila kitu kilikuwa kipya na kigeni kwake; kwa hiyo, alivunjwa vun- jwa moyo humo; alitakiwa afundishwe kazi zake mpya; ali- zoneshwa kama usemi ulivyokuwa.

‘Kuzoesha’ ilikuwa neno lililotumika badala ya nidhamu kali, ambayo ilifikiriwa na wapinzani wa utumwa kubeba si chini ya asilimia ishirini ya wale waliopitia humo. Inawezekana hiyo inazidi kiwango halisi, lakini hata hivyo lazima ikubalike kwamba idadi kubwa walikufa. Nidhamu ilikuwa chungu, hapakuwe- po na nafasi ya kurekebisha kwa kuifanya kuwa nzuri zaidi na asili mia sabini hawakufika mwisho.4

Watumwa walipita kwenye hatua ngumu za mateso ya kuo- gofya na kutisha hasa. Limbikizo la athari za mateso yote zilikuwa msiba mkubwa. Tunamnukuu Sherrard tena, “hii ilikuwa kweli zaidi kwenye mpito wa ‘nidhamu’, kwani bila shaka yoyote sehemu kubwa ya watumwa waliokufa kwenye nidhamu yake wangekufa katika tukio lolote kutokana na athari za mpito wa kati. Uzoefu ulionyesha kwamba idadi kubwa zaidi ya watumwa waliokuwa dhaifu au kukonda wakati walipowasili, walikufa muda mfupi baadaye kutokana na jambo lolote walilofanya. Mamlaka za tiba zilitoa taarifa kwamba hali hiyo ilisababishwa na kufungiwa kwenye nyumba za watumwa kwa muda mrefu kabla ya kupanda meli, haja ya usafi na hewa wakati wapo ndani ya meli, kubadilisha nguo, chakula na tabia, na hasa zaidi mabadiliko ya hewa (Buxton, uk. 188).

Lakini walikubali kwamba palikuwepo na jambo lingine zaidi ya hilo-hujuma ya kisaikolojia au kiroho, ambayo waliielezea, labla kwa namna ya ajabu, kama ‘masikitiko ya kukumbuka ndugu na urafiki, uvunjaji sheria wa kifidhuli wa yale yote yaliyokuwa yanaheshimiwa sana na mapenzi ya kijamii ya nchi na undugu, na matumaini yasiyo na mwisho ya kushushwa daraja ya utumwa kamili.’ Hili likijumlishwa kwenye mateso ya kimwili pia lilivunja utashi wa kuishi na mtumwa alifanya hivyo haraka sana pindi alipopata nafasi ya kwanza, au kwa urahisi zaidi, alijibana na kufa.”

Kwa uchache, walikuwepo wamiliki wa aina tano na sura tano za utumwa wa watu weusi – Kihispania, Kifaransa, Kidachi, Kidenishi na Kiingereza bila kuhesabu Marekani, ambayo mwanzoni ilikuwa Kiingereza. Waamerika ndani ya U.S.A., hadi sasa, karne hii ya ishirini, wanavunja sheria zao wenyewe na mtu mweusi bado hajafuzu kupata haki kamili za uraia, na yapo matatizo kwa Mtu Mweusi (Mnegro) nchini kwake mwenyewe kama dunia ijuavyo fika (vema).

Hatima ya kuogofya ya mtumwa wa shamba ni mbaya – jinsi alivyopigwa chapa kwa chuma chenye moto, alivyolazimishwa kushughulikia minyororo mizito, mgongo wake ulichanika na kuwekwa alama za kuchapwa kwa kiboko, jinsi alivyofungiwa jela w

akati wa usiku, makazi na malazi yake, mara nyingi yamejengwa chini ya ardhi na ni machafu.” Wareno walijenga msululu wa ngome, katika pwani ya Guinea, ambamo Waafrika wanyonge waliwekwa baada ya kukamatwa hadi idadi ilipotimia kustahili kusafirishwa kwenda Hispania, kwenye utumwa na baadaye Marekani na Ulimwengu Mpya…

roho zao zilihukumiwa kwenye mateso ya milele; miili yao ilikuwa mali ya taifa la Kikristo ambao wangekalia nchi yao.”5
Mwandishi anaelezea jinsi utumwa ulivyoanzishwa kwenye makoloni ya Uingereza ndani ya Marekani: “Meli ya Kidachi ilikuwa inaingia kwenye Mto Jame huko Virginia na kupakuwa watumwa weusi ishirini wa kuuzwa. Wakoloni waliwanunua haraka sana na hivyo utumwa wa Mtu Mweusi ukaanzishwa huko kwenye makoloni ya Uingereza yaliyokuwa Marekani.” Kwa kipindi kifupi,” Uingereza ilipata nafasi ya kwanza ya shehena za siri za watumwa, nafasi ambayo ilishikilia kwa kipindi cha zaidi ya miaka tisini.”

Watumwa waliuzwa kwenye minada, walinunuliwa wakiwa uchi wa mnyama, wanaume kwa wanawake wote namna moja, na mtumwa alikalishwa kwenye kiti, ambapo wanunuzi (wazabuni) walimkagua na kushika shika misuli yake na kukagua meno na kumfanya aruke na kunyoosha mikono, ili kuthibitisha kwamba hawakununua mtumwa mgonjwa au asiye jiweza. Kwa kuwa watumwa walinunuli- wa mmoja mmoja, kilichofuata ni kwamba mume na mke, watoto na wazazi walikwenda kwa wamiliki tofauti; na hasara ya ndugu na jamaa na yote yale ambayo watumwa walikuwa wanayapenda yalijumlishwa kwenye hasara ya kukosa uhuru, kwa hiyo mtumwa aliondoka kwenye chum- ba cha mnada, akiwa amenyang’anywa kila kitu, kuanza maisha mapya yalio duni, ya kukata tamaa na utumwa wa kuangamiza.”6

  • 1. Sherrad, B. A., Freedom from Fear (London, 1959) uk. 61-62.
  • 2. Ibid. uk. 67f.
  • 3. Ibid uk. 11.
  • 4. Ibid. uk. 69.
  • 5. Ibid. uk. 26.
  • 6. Ibid uk. 67