Mkakati Wa 7: Kubadili Visomo

Halafu, unahitaji kubadili visomo kwa kusoma Sura tofauti za Qur’an tukufu, du’a tofauti tofauti na nyiradi za namna mbalimbali ndani ya Swala yako. Hili ni muhimu kwa sababu ubongo wako hautakuwa na desturi na mezoea kwa kile kinachosomwa kila siku na kuondoa uangalifu kwa kitu kingine chochote.

Ubongo wa mwanadamu unaweza kushughulikia hali zenye tofauti kwa muda wowote uliowekwa, kwa hiyo unahitaji kuizuia hali hii wakati unapowasiliana na Allah (s.w.t.).

Njia moja ya kuweza kufanya hivyo ni kubadili visomo ili daima uwe mwenye kuzingatia. Kujifunza na kukariri Sura mpya za Qur’an Tukufu, kujifunza du’a na nyiradi mbalimbali, mpya, kwa hiyo, kunapendekezwa sana.

Kwa mfano, kama kwa kawaida unasoma Suratul Qadr baada ya Suratul Hamd katika rakaa yako ya kwanza ya Swala, basi utasoma Suratul Falaq badala yake, au Sura nyingine yoyote kutoka kwenye Qur’an tukufu. Kwa vile hii ni Sura mpya kabisa, akili yako haitaruhusu mawazo yoyote yanayopotoka kwa vile imeshughulishwa na kulengwa kwenye kumaliza hiyo Sura mpya.
Hali kadhalika, kama unasoma du’a maalum katika Qunut yako, tumia muda kujifunza du’a mpya tofauti tofauti na uzisome katika Swala yako. Vilevile, kama umezoea kusoma dhikr katika sajidah yako ya mwisho, kwa nini usijaribu kuwa na visomo hivi katika sajidah zako za awali pia – dhikr tofauti wakati wote? Lazima tuwe waangalifu hata hivyo, kwa sababu katika masuala mengine kama vile Tashahudi, Salam na vitendo vingine katika swala, huwa haturuhusiwi kuongeza au kubadili vile visomo vya wajibu.