Mkakati Wa 15: Kuweka Mawazo Kwenye Maandishi

Kwa bahati mbaya sana, katika hali yoyote ya utulivu hasa Swala, ni suala la kibinadamu kuwa na idadi ya mawazo bunifu, na vilevile kumbukumbu ya mambo uliyosahau au unayohitaji kufanya. Mawazo haya yanaweza kuisumbua tafakari yako endelevu kama hutayaandika.

Imeshauriwa na wanavyuoni wakubwa wakubwa kuyaandika mawazo haya kwenye kipande cha karatasi ili uiweke huru akili yako kuweza kumakinika kwenye swala.
Unaweza kwa hiyo kuendelea kwa urahisi zaidi bila ya kung’ang’ania kwenye mawazo unayohofia kwamba unaweza kuyasahau. Utakuwa unaleta akili yako ya ufahamu na yaliyofichika akilini mwako karibu kwa pamoja na hili litazalisha taarifa za maana na mawazo utakayotaka kuyafuatia baada ya kumaliza swala yako. kwa maelezo zaidi tafadhali rejea Kitabu cha mazoezi ya siku thelathini.