Kundi La Tatu: Kujitathmini Mwenyewe:-

Mara tu, pale utakapokuwa umekamilisha zoezi lako, Swala ya rakaa 4, utapima yafuatayo katika chati yako binafsi – umakinifu, nishati na motisha.

Umakinifu – uwezo wako wa kulenga na kujihudhurisha kwenye Swala.

Nishati – uwezo au juhudi; moyo wa kupenda kutekeleza Swala. Motisha – ni namna fulani inayoingilia kati au hali ya ndani ambayo inakuhimiza au kukusukuma kwenye Swala.

Kichangamsho cha tabia.

Hii namba 10 ni – vizuri sana na ndio ushindi hesabu bora kabisa ya ushindi unayoweza kujipa mwenyewe, sifuri ni hesabu ya chini kabisa, na namba 5 ni wastani.

Pima kiwango chako cha UMAKINIFU wakati wa Swala

1 5 10

Pima kiwango chako cha NISHATI wakati wa Swala

1 5 10

Pima kiwango chako cha MOTISHA wakati wa Swala

1 5 10

Andika yale mawazo yote yanayopotosha ambayo ni dhahiri yalikuathiri na ni mara ngapi yalijirudia:
Ni mara ngapi ulipotoshwa kwa dhahiri katika Swala yako?

Je! Ulikwisha kuyalipa madeni yote kwa Allah (s.w.t.) kama ulivyokuwa umeahidi (wakati na baada ya Swala yako ya kawaida)? (MCHORO WA NNE).

Unaweza sasa kuzipanga chati zako kwa mpango. Unazo chati 4 mwishoni mwa ZOEZI hili – UMAKINIFU, NISHATI, MOTISHA NA MADENI. (MCHORO WA TANO)