Aya 19 – 22: Mwenyezi Mungu Ni Mpole Kwa Waja Wake
Maana
Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku ampendaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.
Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametaja kuwa Yeye ni mpole Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu na Mwenye kushinda. Makusudio ya upole ni kufanya wema. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ {28}
Maana ya kuruzuku ni kuwa Mwenyezi Mungu anampa mtu nguvu zote za maandalizi ya kufanya kazi ya kupata riziki na kumuongoza kwenye njia yake, kuongezea kuwa kheri zote zilizo ardhini na mbinguni ameziten- geneza Yeye kwa ufadhili wake. Ama kuwa na nguvu na kushinda ni kuwa Yeye hashindwi na lolote wala hakuna kitu asichokiweza ardhini au mbinguni.
Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu.
Mwenye kuitumikia Akhera atapata malipo ya aliyoyafanya na Mwenyezi Mungu atamzidishia ziada nyingi tu, na hatapunguziwa kitu duniani.
Hakuna mwenye shaka kwamba kufanya bidii kwa ajili ya maisha ni katika kuitumikia Akhera vile vile, lakini mwenye kuitumikia dunia peke yake na kuiacha Akhera, atastarehe siku kidogo tu, kisha atahamia kwenye adhabu ya daima. Watakokuwa na hali mbaya zaidi ni wale wanaoifanyia biashara dini na kuitafuta dunia kwa kazi ya Akhera kiunafiki na ria.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:145), Juz. 15 (17; 18-19).
Au wana washirika waliowawekea dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu?
Ni swali la kukana na kutahayariza. Makusudio ya washirika ni mashetani watu na majini. Kuwawekea ni kuwadanganya na kuwapambia pambia. Maana ni kuwa, kwa nini wakosefu wanaitumikia dunia na kuisahau Akhera? Je, ni kwa kuwa wana mashetani wanaowazuia nayo kwa kuwatia wasiwasi na mambo yasiyokuwa kwenye dini?
Kisha Mwenyezi Mungu amewatishia kwa kusema: Na lau lisingekuwako neno la kupambanua basi wangelikatiwa hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu.
Hekima Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu imetaka kuiahirisha adhabu ya wakosefu hadi siku ya ufufuo; vinginevyo angelimpatiliza kwa adhabu kila mkosefu mwenye dhambi.
Utawaona hao madhalimu wanavyokuwa na hofu kwa sababu ya waliyoyachuma, nayo yatawafika tu. Na walioamini na wakatenda mema watakuwamo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao. Hiyo ndiyo fadhila kubwa.
Kesho itapita hisabu kwa matendo yote. Mwenye kutenda mema atakuwa katika amani na Pepo, humo atapata kila analolipenda na kulitaka; na mwenye kufanya maovu atakuwa katika hofu ya hasira za Mwenyezi Mungu na adhabu yake. Adhabu hiyo itamfika tu, ikiwa ni malipo kwa iliyochuma mikono yake.
Nitii Utakuwa Mfano Wangu
Hapo mwanzoni nilikuwa nikizitilia shaka Hadith mbili nilizokuwa nikizisikia mara kwa mara masikioni mangu: Ya kwanza ni Hadith Qudsi isemayo: “Ewe mja wangu nitii utakuwa mfano wangu, utakiambia kitu kuwa na kinakuwa.” Na nyingine ni ya Mtume isemayo: “Hakika Mwenyezi Mungu ana waja wakitaka naye hutaka.”
Nilikuwa nikitilia shaka mategemezi ya Hadith mbili hizi, kwa vile sikuzionea athari yoyote katika maisha haya. Kisha nikagundua, wakati nikifasiri Aya za Qur’an yenye hekima, kuwa maudhui ya Hadith hizi ni ya Akhera si ya dunia, basi shaka yangu ikaniondokea na nikawa na yakini kuwa Hadith mbili hizi ni tafsiri na ubainifu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na walioamini na wakatenda mema watakuwamo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao.’
Na mfano wa Aya hiyo.
ذَٰلِكَ الَّذِي يُبَشِّرُ اللَّهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۗ قُلْ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ ۗ وَمَنْ يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ شَكُورٌ {23}
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا ۖ فَإِنْ يَشَإِ اللَّهُ يَخْتِمْ عَلَىٰ قَلْبِكَ ۗ وَيَمْحُ اللَّهُ الْبَاطِلَ وَيُحِقُّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ {24}
وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ {25}
وَيَسْتَجِيبُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَيَزِيدُهُمْ مِنْ فَضْلِهِ ۚ وَالْكَافِرُونَ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ {26}