read

Maisha Ya Mtume Saleh

Mtume Saleh a.s. aliitwa:

Mtume Saleh a.s. bin Abud bin Asif bin Nasikh bin Abud bin Hadir bin Thamud bin Amir bin Sam bin Nuh.

Kabila lake lilikuwa likiishi mipaka ya Kusini ya Syria katika milki iliyokuwa ikijulikana kama Al-hijr au Al-Hajar na ilijulikana kama Wadi-ul-Qura.

Mtume Saleh a.s. alikuja baada ya Mtume Hud a.s. na alitokana na kizazi cha tisa cha Mtume Nuh a.s.

Urithi

Baada ya kuangamiza Allah swt Qaum-u-‘Aad ambao hawakuyasikiliza maneno ya Mtume wao Hud a.s. na baada ya kufa hao wote ikabaki ardhi yao bila majumba wala wakazi wala mimea hata wanyama na baada ya haya yote Allah swt aliirithisha ardhi yao kwa Qaum nyingine nao ni Qaum Thamud. Wakaja Qaumu Thamud mahali pakawa Qaum-u-‘Aad Allah swt aliwaneemesha neema nyingi kuliko Qaum ‘Aad.

Walijenga Qaum Thamud majumba kati ya majabali na wakalima mabustani na makonde na wakatoboa mito lakini pamoja na masikitiko makubwa hazikuwa akili zoa zina maendeleo kuliko Qaum iliyotangulia.

Ni hao hao ambao waliabudu masanamu na mawe na wakadhani kwamba neema yao haitoondoka na wala haitatoweka.

Ujumbe

Na mbele ya utakafiri huu na ujinga Allah swt alimtuma kwao mwanamme miongoni mwao anayeitwa Mtume Saleh a.s. na yeye miongoni mwa watukufu wao na mwenye akili katika wao ambaye alimuamini Allah swt wake na Allah swt alimchagua yeye ili awaongoe hawa Majahili waliopotea akawalingania wao kwenye ibada ya Allah swt na akatilia mkazo na akawaimiza wao juu ya Tawhid yaani kumpwekesha Allah swt na kuacha kumshirikisha Yeye ni Yeye ambaye aliwaumba wao na akawaumbia wao ardhi na akawapa wao miongoni mwa fadhila Zake na neema Zake kisha akawakataza wao kuabudia masanamu ambayo wameyatengeneza wao wenyewe.

Kwani hayo masanamu hayadhuru wala hayanufaishi chochote na wala hayamtoshelezi mtu kutoka kwa Allah swt chochote kisha akawakumbusha wao kwamba yeye ni miongoni mwa wao na yeye anapenda kuwanufaisha wao na wanapojipatia maslaha yao na akawaamrisha wao wamtake msamaha Allah swt na watubu kwake Yeye kwani yeye ni mwenye kusikia na mwenye kujibu na anakubali toba kwa yule mwenye kutaka msamaha kwake.

Upingaji

Lakini masikio hayakusikiliza wala nyoyo hazikufunguka na macho hayakuona wakapinga na kumpinga Mtume Saleh a.s. pamoja na ujumbe wake na wakawa wanamfanyia mzaha kwa ujumbe wake na wala hawakusimama kwao ukafiri mpaka kufikia kiwango hiki bali walisema kumwambia Mtume Saleh a.s.:

“Ewe Mtume Saleh a.s. sisi tumekujua wewe kwamba ni mwenye akili na mwongozi na tulikuwa tunakuuliza wewe na tulikuwa tunakutaka ushauri wewe katika mambo yetu una nini leo unatamka mambo ya upuuzi na upi huu msamaha ambao wewe unatuitia sisi kwao aidha sisi tunaabudu walichokua wanaabudu mababa zetu miongoni mwa masanamu na miungu aidha sisi hivi sasa tupo katika shaka kwa kile unachotuitia sisi kwacho na wala hatutaamini maneno yako na wala hatutosadiki na kuacha itikadi zetu na itikadi za mababu zetu kwa ajili yako.”

Kutahadharisha

Aliposikia Mtume Saleh a.s. kutoka kwao maneno haya aliwajibu wao kwa hali ya subira na kihekima akisema:

“Enyi watu hakika ambayo nayasema ni haki na hakika ya mnacho kiabudu miongoni mwa mawe ni batili na hakika mimi naogopa kwenu kutokana na nguvu za Allah swt ambaye mnamkufurisha baada ya kukupeni nyinyi mali na majumba na mabustani.

“Enyi watu mtakeni msamaha Allah swt hakika mimi ni mjumbe wa Allah swt kwenu wala sitaki kwa nyinyi mali wala urais hakika si jambo lingine nachotaka mimi ni kukuongoeni nyinyi na kujalieni nyinyi mfikiri na malipo yangu mimi yapo kwa Allah swt Bwana wa viumbe wote ambaye amenituma mimi kwenu na yeye ambaye atanilipa mimi Akhera na ataneemesha kwenu neema nyingi ikiwa nyinyi mtajibu na kukubali Da’awa yangu kwa imani na kwa kusilimu.

Wanyonge

Na katika kila kaumu enyi ndugu zangu hupatikana watu wenye akili na ambao wanapenda nasiha na katika Qaumu ya Thamud kulikuwa na kikundi cha watu wachache miongoni mwa watu wanyonge ambao waliona kwamba utajiri haunufaishi chochote mbele ya ujahili wakafikiria kwa akili zao wakaona kwamba hakika anachowaitia Mtume Saleh a.s. ni cha haki na kuingia akilini.

Hakika Allah swt ameumba ulimwengu na masanamu hayanufaishi chochote japokuwa waliabudia hayo masanamu mababa na mababu vikafunguka vifua vya kikundi hiki cha watu wachache na wakaingia katika dini mpya na wakatangaza kusilimu kwao na wakaingia katika imani na kwa hali hii wakawa pamoja na Mtume Saleh a.s. baadhi ya watu walio amini miongoni mwa kaumu yake walioshudia kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah swt na kwamba yeye Mtume Saleh a.s. ni mjumbe wa kutoka kwa Allah swt .

Subira na Jihadi

Na ama ambao waliofanya kiburi na wakazuia Da’awa ya Mtume Saleh a.s. kwa vitimbi vyao na wakashikamana kwa ibada zao za kuabudu masanamu na wakamwambia Mtume Saleh a.s. kwamba hakika Shetani amekutania wewe na ukawa unatamka mambo ya wazimu kisha wakawa wanamzuia yeye kunako dini yake lakini yeye alisubiri na akavumilia kutokana na maudhi yao na vitimbi vyao na akaendeleza tablighi yake na akasema :

“Enyi watu hakika mimi sikuacha dini ya haki na nikakufuru kama mlivyo kufuru nyinyi na wala hamtoweza kurudisha kwangu mimi adhabu inayotoka kwa Allah swt .”

Lakini ikiwa mmeingia katika Uislam na mkapata uongofu na imani hakika Allah swt atakuingizeni nyinyi baada ya kuamini kwenu Jannat (peponi) siku ya Qiyama.

Enyi watu hamkuwa nyinyi isipokuwa ni waongo mnaacha kutumia akili zenu na mkafata matamanio yenu na mkawa miongoni mwa makafiri.

Hofu

Na walipo kutakwamba imani imepata nguvu na subira na mshikamano wenye nguvu waliogopa Mustakbirun kwamba kikundi cha waumini wachache kitazidi na kuwa chenye nguvu hakika waliogopa enyi ndugu zangu juu ya mali zao na maslaha yao na wakaogopa juu ya dola yao na ufalme wao basi vipi wataishi kesho ikiwa idadi ya Muumina itaongezeka.

Hakika hakuna budi ila kuondoa mushkili huu walifikiri makafiri juu ya jambo hili ambalo lilikuwa linawahuzunisha wao na serikali yao wakaona kwamba wamuombe Mtume Saleh a.s. baadhi ya mambo ayafanye wakidhani kwamba hatoweza kuyafanya hayo mambo na baada ya hapo watajitenga watu ambao walioamini baada ya kudhihiri kushinda kwake na udhaifu wake.

Kuomba muujiza

Na kawaida ya makafiri ambao hawaamini wao hupenda kuwatenganisha watu kutoka kwenye imani ili wawe kama wao na walidhani hawa makafiri kwamba makafiri kutoka kaumu ya Mtume Saleh a.s. kwamba watakapo mtaka Mtume wao jambo gumu na atakapo shindwa kulifanya hakika wanachomtakia wao kitakuja kuthibitika. Na watakuja hao makafiri kwa Mtume Saleh a.s. wakizungumza naye kuhusu muujiza wake na wakimtaka awaletee wao huo muujiza ili hiyo dalili juu ya ukweli kwa jambo lake na kwamba yeye ni mtume wa Allah swt kama wanavyodai kwake. Na hakika walisema kwamba watakapo taka tukuamini wewe na kuamini ujumbe wako tuletee muujiza ili tukuamini la sivyo sisi tutabaki katika ibada yetu ya masanamu.

Ngamia

Hakika ya Mtume Saleh a.s. hawezi kufanya jambo lolote isipokuwa kwa idhini ya Allah swt na vipi ataweza kufanya jambo na yeye ni mtu kama wao. Hakika Allah swt enyi ndugu zangu anajua kwamba makafiri wengi hawaamini hata kama wataona muujiza lakini ili uwe ukafiri wao ni hoja iliyo batilika hakika Allah swt alituma kwao Ngamia wa ajabu na muujiza wa Ngamia huyu kwamba yeye anakunywa maji siku moja na kujizuia kunywa maji siku ya pili na akasema Mtume Saleh a.s. kuwaambia kaumu yake kwamba huyu Ngamia amemtuma Allah swt na atakuwa kinywaji chake katika kijiji ni cha kupokezana siku moja ni yenu nyinyi na siku moja ni yake yeye. Jiepusheni na kumuuzi Ngamia huyu na msibadilishe amri na nidhamu hii.

Hofu kutoka kwa makafiri

Na hakika Mtume Saleh a.s. alijua kwamba makafiri imewaogopesha amri hii ya Allah swt kwa hivyo watafanya njama ya kumuua Ngamia.

Kwa sababu hiyo alikwenda Mtume Saleh a.s. kwa kaumu yake na yeye akiwaambia kwamba (msimfanyie mabaya Ngamia huyu na mtakapo muudhi Ngamia huyu basi Allah swt atashusha adhabu juu yenu kwa haraka). Hakika amewafikishia Mtume Saleh a.s. ujumbe na akawatahadharisha wao na akawaonya lakini makafiri waliona kwamba huo muujiza uko wazi na unajulisha wazi Utume wake, wakaogopa isije ikazidi idadi ya walioamini na wakaongezeka waliokuwa pamoja na Mtume Saleh a.s., basi wao yaani makafiri hawapendi watu waamini au waamini mwingine zaidi ya walioamini kwa sababu hiyo kwamba wao walifikiri katika njia nyingine kinyume cha Mtume Saleh a.s. na sasa hawataki tena muujiza mwingine na kwamba wao walikengeuka kwenye kitu kingine.

Njama

Hakika waliangalia makafiri kumwangalia Ngamia mnene wa ajabu wakaogopa juu ya serikali yao kutokana na muujiza huu ulio wazi na wadhahiri na kwamba muujiza huu unavuta nyoyo za watu na unazivutia nafsi za watu. Yote haya yaliwafanya wao wafikirie juu ya muujiza huu nao ni Ngamia kwamba ni muujiza wa hatari na wao hawawezi kuepuka hatari hii ila kwa kumuua Ngamia, wakafikiria mbinu ya kutimiza njama zao na mwisho wakaafikiana kwamba waende baadhi yao mahali anaponywea maji Ngamia na huko huko watamwulia wakati Ngamia anaporejea kutoka mahali anaponywe maji na wao watakuwa wamejiepusha na muujiza huo wa Mtume Saleh a.s. wenye kutisha na kuogopesha.

Mapambano ya Ngamia

Moja kwa moja kikatoka kikundi cha makafiri kikaenda zake hadi kwa Ngamia wakisubiri marejeo yake kutoka mahali anaponywea maji na wakati alipokuwa akirejea Ngamia, akatupa mmoja wao kumtupia Ngamia mshale ambao ulimchoma na akaanguka Ngamia juu ya ardhi na wala hakutosheka na hayo bali wakamchinja ngamia na kumuua kisha wakarudi kumwendea Mtume Saleh a.s. huku wakisema kwamba hakika ulitutahadharisha sisi na adhabu ikiwa tutamuua Ngamia, tuletee adhabu ! Haya hatutarudia kukuogopa wewe wala Ngamia wako. Mtume Saleh a.s. akawajibu fanyeni starehe zenu kabla ya adhabu ya Allah swt na mateso, hakika nilikutahadharisheni kwa kutokumuua Ngamia na mkamuua basi subirini adhabu iliyo ahidiwa na Allah swt .

Maiti zilizoganda

Hakika ahadi ya Allah swt ni kweli na adhabu ni karibu, kisha makafiri wakamuomba Mtume Saleh a.s. afanye haraka au aharakishe adhabu kwao na wao waliyasema haya katika hali ya kumfanyia mzaha Mtume Saleh a.s. wakaafikiana makafiri upya kwamba wamuue Mtume Saleh a.s. na watu wake wakiwa wao usingizini usiku, lakini Allah swt hakusahau na wala hakumsahau Mtume wake aliye muumin na walioamini pamoja waliomwamini Mtume Saleh a.s. na ulipoingia usiku ikaja ahadi ya Allah swt na adhabu yake ukavuma upepo mkali ulio mkubwa na wenye kutisha ukawafanya makafiri kuwa ni miili iliyoganda haitikisiki abadan, akaamka Mtume Saleh a.s. na akaona yaliyo pita juu ya makafiri na akajua kwamba Allah swt amesha wateketeza na kuwaangamiza wao, na Allah swt akamwamsha Mtume Saleh a.s.

Na yeye akawaamsha wale waliokuwa wamemwanini yeye na akasema:

“Enyi watu wangu! Hakika nimekufikishieni nyinyi ujumbe wa Allah swt na nikakuonyeni lakini hamuwapendi wenye kutoa nasiha.”

Mwisho

Na sasa je mmeona enyi ndugu zangu vipi kafiri asiyamini vile muujiza usivyomfaa yeye chochote na anavyouogopa ?

Nao waliomba muujiza kutoka kwa Allah swt naye akatuma Ngamia na Mtume Saleh a.s. akawatahadharisha wao wasimwudhi Ngamia na wao wakamwudhi na vile vile wakamwua na Mtume Saleh a.s. aliwatahadharishia adhabu, wao wakaiomba adhabu na kisha Mtume Saleh a.s. akawaahidi wao adhabu na wakasema iletwe haraka kwao.

Je walipata faida yoyote kutoka kwa muujiza ?

Jibu ni kwamba wao hawakufaidika chochote.