read

Yajuj Na Majuj

Allah swt anasema katika Quran, Sura Al-Kahf, 18, Ayah 92 - 99.

Kisha akaifuata njia.

Hata alipofika katikati ya milima miwili,alikuta nyuma yake watu ambao waliweza kwa shida kufahamu neno (wanaloambiwa).

Wakasema:“Ewe Dhulqarnain! Hakika Yajuj na Majuj wanafanya uharibifu katika ardhi.Basi je,tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?”

Akasema:“Yale ambayo Allah swt wangu amenimakinishia ni bora (kuliko ujira wenu.Nitakufanyieni bure);Lakini nisaidieni kwa nguvu zenu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi chenye imara.”

Nileteeni vipande vya chuma.” Hata alipoijaza nafasi iliyo katikati ya milima miwili,alisema:“Pulizeni”mpaka alipokifanya (kile chuma) kuwa moto,alisema “Nileteeni shaba iliyoyayuka niimwage juu yake.”

Hivyo (Yajuj na Majuj) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa.

Akasema:“Hili ni rehema itokayo kwa Allah swt wangu.Na itakapofika ahadi ya Allah swt wangu ya kufika Qayama), atauvunjavunja. Na ahadi ya Allah swt wangu ni kweli tu.”

Yajuj na Majuj walikuwa ni viumbe vyenye miguu minne na wakifanana na wanaadamu kisura na wao walikuwa ni wafupi mno mbele ya watu wa zama hizo. Na watoto wao walikuwa wakizaliwa kama watoto wa wanaadamu na walikuwa hawakui zaidi ya shubiri tano na sura zao zilikuwa aina moja na walikuwa wazururaji.Kwa kuwa ngozi zao zilikuwa ngumu kama zile za ngamia, hivyo hawakuathirika kwa baridi wala joto. Walikuwa na makucha makubwa na meno makali na masikio yao yalikuwa marefu kiasi kwamba walikuwa wakitandika moja na kujifunika kwa la pili. Walikuwa wakiingiliana kama wanyama na chakula chao kikubwa kilikuwa ni samaki kwa sababu kulikuwa kukinyesha mvua za samaki, na kama kulikuwa na kasoro ya samaki basi walikuwa wakishambulia miji na kuchafua na kuvuruga kila kitu kiasi kwamba watu walipokuwa wakizisikia sauti zao,walikuwa wakikimbia na kuacha makazi yao kwa sababu ilikuwa ni vigumu mno kuwakabili kwani walipokuwa wakiingia mijini basi miji yote ilikuwa ikijaa wao tu. Idadi yao ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba hakuna mtu mwingine ajuaye isipokuwa Allah swt . Wao walikuwa hawafi hadi wamezaa watoto zaidi ya elfu moja.

Katika vitabu tunapata habari zaidi kuwa Yajuj na Majuj ni makabila mawili yaliyokuwa makubwa kutokana na kizazi cha Yafus, mwana wa Mtume Nuh a.s.. Na katika Agano la Kale, Majuj anaelezwa kuwa ni Chifu wa Mashech na Tunal. Kwa sasa Moscow ndio mto unaosimama mji huo,uitwao Moscow, mji mkuu wa Urusi; Tabul ni mto huko Urusi ambapo kuna mji Tobolsk.

Katika eneo la Ulaya ya Kusini na Urusi ya Kiasia,baina ya Wacarpathiani na Don, kulikaliwa katika enzi za zamani na kabila katili kabisa ambao waliiteka Asia ya Magharibi kuanzia karne ya 7 Kabla ya Kristo hadi mwanzoni mwa kipindi cha Kikristo, wakati mashambulizi yao yalipokwisha kwa sababu ya Bwana Dhulqarnain alipoujenga huo ukuta.

Vile vile inasemekana kuwa neno Mongol ni mvurugano wa neno la Kichina Mongog au Manchog Iwapo utafiti huu utakuwa wa kweli,hivyo. Hivyo itamaanisha kuwa eneo la Yajuj na Majuj inaanzia Mto wa Moscow hadi Turkistan ya Kichina na Mangolia.

Maelezo ya ‘kuta’ katika Quran Tukufu yanaonyesha kuwa lazima iwe imejengwa pale penye njia ili kuzuia makabila hayo ya wachochezi na wakatili kuwashambulia majirani wao waliokuwa mafundi stadi katika kazi za kufua vyuma na walikuwa matajiri.

Sheikh Abul-Kalam Azad,katika moja ya makala yake (katika Jannatul-Ma’arif) anaelezea kuwa kuta hizo zimeendelea hadi Uturuki.

Ayatullah Agha Haji Mirza Mahdi Puya Yazdi (katika hashia ya Tafsiri ya Quran iliyofanywa na S.V. Mir Ahmad Ali) anawanakili wengine wakisema kuwa kuta hizo zipo baina ya milima ya Armenia na Azerbaijan.

Hata hivyo kuna tofauti ya maoni kuhusu utambulisho wa Dhulqarnain. Bwana ‘Abdullah Yusuf Ali anadhani kuwa jina hilo linaelezea kuwa ni Alexandar Mkuu wa Misri.

Wengineo,kama Agha Puya, wanafikiri kuwa huyo anatambulishwa kama ni Mfalme wa Kiajemi aliyekuwa akiitwa Darius.

Kwetu sisi hatumaanishi kuingia katika mazungumzo mengi kuhusu mjadala huu lakini inatubidi liwe jambo lililowazi mbele yetu kuwa kwa mujibu wa Quran Tukufu, Dhulqarnain alikuwa ni mcha Mungu hivyo kamwe haiwezekani kumtambulisha Dhulqarnain kama kafiri au mpagani.

Kwa mujibu wa Quran Tukufu,Itakapokaribia Siku ya Qayama, kabila hizi zitafanikiwa kuvunja kuta, yaani zitaenea zaidi kuliko mipaka yao ya awali.Upanuzi huo unaweza kuwa kimantiki;ambapo inaweza kumaanisha kuwa itikadi zao (ukomunisti na ukafiri) zinaweza kuenezwa nje ya mipaka ya nchi zao. Au itakuwa aina ya kikoloni yaani kukalia maeneo ya mashariki ya Ulaya,Asia ya Kusini na maeneo mengineyo. Au inaweza kumaanisha yote.

Imeandikwa katika Tafsir Majma’-ul-Bayan kuwa baada ya kuteka maeneo ya ardhi watajararibu kuiteka mbingu.“Hivyo watatupa mishale yao kuelekea angani,na itawarejea zikiwa na alama kama za damu. Hivyo watasema:‘Sisi tumekwishawateka wakazi wa dunia na tumewateka wakazi wa angani.”

Ni dhahiri kuwa mishale inamaanisha maroketi na vyombo vya angani. Maneno itawarejea zikiwa na alama kama za damu inamaanisha kuwa vyombo vya angani vitafikia malengo yao na kurejea duniani.

Kwa mujibu wa Tafsiri hiyo,“wakati watakapokuwa na takabari kubwa kwa sababu ya kushinda anga za juu, Allah swt atawaumba funza au minyoo ambayo itawaingia masikio yao, na kuwaua wote.Inamaanisha kuwa hatima yao itakuwa kwa kuangamizwa kwa maafa makhsusi, au kwa magonjwa ya kuambukizwa yatakayotokana na vijidudu.