Katika Uislamu ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kutokana na umuhimu wake katika kuijenga na kuiendeleza jamii.
Taarifa za ndani ya kitabu hiki cha mwongozo zimeegemea kwenye vyanzo sahihi na vya asili vya mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake (a.s). Na ingawa kimeandikwa kwa mtazamo wa Kiislamu, lakini ni kitabu ambacho kitawafaa sana hata wasio Waislamu, kwani kinazungumzia maisha ya ndoa kwa ujumla.