Aya 61: Na Mliposema

Na mliposema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia kwa chakula cha namna moja tu.

Yaani walisema wahenga wenu walipokuwa katika kuhangaika, walipochoka kuendelea kula Manna na Swala, wakapendelea masiah yao ya mjini, Hakuna kosa hapa katika matawa yao, Kwani kila mtu anapendelea namna mbali mbali ya chakula, hali hiyo ndiyo inayoleta matamanio. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amehalalisha riziki njema kwa waja wake. Kwa hivyo Aya haiko katika mfumo wa kutusi bali ni kustaajabu kukataa kwao maisha yasiyo na tabu na kutaka maisha ya dhiki na usumbufu.

Akasema: Mnabadili vitu duni kwa vile vilivyo bora?

Herufi ‘ba’ (kwa) inaingia kwenye kitu bora, sio duni, Tunasema: Usibadilishe shaba kwa dhahabu, hatusemi: Usibadilishe dhahabu kwa shaba,” lakini watu hufanya kinyume, kwa vyovyote itakavyokuwa muhimu ni kujua makusudio.

Nendeni kwenye mji; huko mtapata mlivyoviomba.

Yaani Musa ndiye aliyewaambia hivyo. Kwa dhahiri makusudio ya neon Misri ni mji kwa sababu Mwenyezi Mungu hakubainisha mji maalum. Na tafsiri ya Quran siyo ya kinahw ambayo itasahihishwa na Sibawayh na Naftawayh.

Na ikapigwa juu yao (chapa ya) udhalili na umaskini.

Walikuwa watukufu walio huru; riziki ikiwajia maridhawa, wakakataa isipokuwa kulima, uhunzi na biashara. Yote hayo yanaleta mashindano na vita ambavyo vinaleta kuhemewa na kukosekana amani.

Na wakiwaua Manabii paispo haki.
Kwa dhahiri kuwaua Manabii kunakuwa bila ya haki. Kama kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu (s.w.t.) aliwasuta na kuwambia kwamba kuua, kwao hakukuwa kwa kukosea, bali ni kwa makusudi na inadi tu. Kwa hiyo hakuna geni kwa vitendo vya mayahudi, kwa sababu hiyo ndiyo asili yao.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ {62}

Hakika wale ambao wameamini na Mayahudi na Manaswara na Wasabai; yeyote atakayeamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akafanya vitendo vizuri basi watapata malipo yao kwa mola wao, wala haitokuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika.