Aya 76-77: Wanapokutana Na Wale Walioamini

Maelezo

Baadhi ya Mayahudi walikuwa wakifanya unafiki na uwongo kwa Waislamu na wakisema: “Sisi tunaamini yale mnayoyaamini nyinyi na tunashuhudia kuwa Muhammad ni mkweli katika maneno yake, kwani tumekuta katika Tawrat sifa zake.

Lakini wanafiki hao wanapochanganyikana na viongozi wao, basi viongozi wanawalaumu kwa kusema: “Vipi mnawahadithia wafuasi wa Muhammad yale aliyowahukumia Mwenyezi Mungu? Hivi hamfahamu kwamba huko ni kukubali nyinyi wenyewe kwamba mko katika batili na wao wako katika haki?”

Hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyafanya siri na wanayoyadhihirisha?

Yaani kwa vyovyote watakavyojaribu wanafiki, kuficha unafiki wao na viongozi wapotevu wanavyowaelekeza wafuasi wao, lakini kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakifichiki chochote. Basi nyinyi Mayahudi mnaficha njama zenu, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamfahamisha Mtume wake Muhammad (s.a.w.) na anavifagia vitimbi vyenu.

وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ {78}

Na wako miongoni mwao wasiojua kusoma; hawajui kitabu isipokuwa matamanio tu nao hawana isipokuwa kudhani tu!

فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَٰذَا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَهُمْ مِمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَهُمْ مِمَّا يَكْسِبُونَ {79}

Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao. kitabu kwa mikono yao. Kisha wakasema hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu ili wachukue kwacho thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao. Na ole wao kwa yale wanayoyachuma.