Aya 101: Walipojiwa Na Mtume

Maelezo

Na walipojiwa na Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Ambaye ni Muhammad (s.a.w.); aliyepelekwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wote wakiwemo Mayahudi waliokuwa zama zake.

Mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nao.

Yaani kusadikisha yaliyo katika Tawrat miongoni mwa misingi ya Tawhid na bishara ya Muhammad.

Kikundi kimoja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu.

Nao ni wanavyuoni wa Kiyahudi.

Kilitupa kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao.

Makusudio ya Kitabu, cha Mwenyezi Mungu, ni Qur’an. Imesemekana pia kuwa ni Tawrat, kwa sababu kumkana kwao Muhammad ni kuikana Tawrat ambayo imetoa bishara ya kuja Muhammad (s.a.w.). Hapa wanaingia wote Mayahudi na Manaswara.

Kwani wote wamekipotosha Kitabu, hasa sehemu zile zinazofungamana na bishara ya kuja Muhammad (s.a.w.); Bali hakuna tofauti kati ya Mayahudi na wale wanaoondoa maneno ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata mapenzi yao.

وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنْزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُمْ بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنْفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنْفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ {102}

Wakafuata yale yaliyofuatwa na mashetani, katika ufalme wa Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi na yaliyoteremshwa kwa Malaika waili, Haruta na Maruta, katika (mji wa) Babilon Wala hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni fitna (mithani), basi usikufuru. Wakajifunza kwao mambo ambayo kwayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawakuwa wenye kumdhuru yoyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatakayowadhuru waka hayawanufaishi. Na kwa hakika wanajua kwamba aliyeyanunua haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera. Na hakika ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao laiti wangelijua.