Kuhusu Wachapishaji

Leo hii akili yenye hadhari inaona kiakili mabadiliko ya maisha ya mwanadamu. Sayansi na teknolojia na mafanikio yao ya kushangaza yanaonekana yamefika kwenye kilele chao. Mahitaji ya kidunia hisia kali za matamanio ya mamlaka na ukubwa, ni mambo ambayo yamemwelekeza mwanadamu kwenye muflisi wa maadili mema.

Katika hali hii ya kukatisha tamaa, mtu analazimika kutulia na kukadiria upya hatari zinazoweza kuwa tishio kwa mwanadamu kwa ujumla. Mwanadamu kwa mara nyingine tena ameelekeza macho yake kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu kwani sasa ametambua kwamba ufumbuzi wa matatizo yake na hatima ya ukombozi wake ni mambo yaliyomo katika kufuata na kutekeleza.

Kuhama huku kutoka kwenye fikra ya mambo ya kidunia na kwenda kwenye mambo ya kiroho ni hali inayoafikiana kikamilifu na malengo na madhumuni ya seminari ya Kiislamu.

Miongozo ya kidini, iliyo sambamba na maendeleo ya wakati uliopo, yanatoa kimbilio linalohi- tajiwa sana na akili inayosumbuliwa na yenye wasi wasi. ni matokeo ya ongezeko la utambuzi, kwamba imeeleweka kwamba siri ya kuishi maisha ya uadilifu hapa duniani kuelekeza kwenye furaha kamili ya milele ya maisha ya Peponi. Huu ni ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu wote.

Jumuiya yetu ya Kiislamu inataka kunyanyua juu mwenge wa mwongozo wa kiroho na kusaidia kwa moyo wote kutangaza urithi wa kiroho wa mwanadamu. Inaonyesha njia ya maisha kwa mujibu wa Quran katika utukufu wake ulio safi kabisa. Inaonyesha hayo tu yenye mamlaka na yaliyothabiti. Uenezi wake umebuniwa kwa jinsi inayoweza kukidhi mahitaji ya kiroho katika wakati uliopo.

Itahudumia kama chemchem ya kudumu kwa wale wenye kiu ya ujuzi. Seminari ya Kiislamu ni taasisi ya kimataifa ambayo inajaribu kuleta udugu wa Kislamu. Inapata mchango mzuri sana kutoka kwa wanachuo, kama nyongeza ya kuwa na msaada wa kimataifa kwa ajili ya kutimiza lengo lake kubwa. Inayo vituo; Asia, Afrika, Ulaya, Amerika, Canada na Mashariki ya mbali.

Mpendwa msomaji.

Kitabu hiki kimechapishwa na Seminari ya Kiislamu. Uenezi wake umebuniwa kwa ajili ya kuhudumia mahitaji ya kiroho katika kipindi hiki ukiwa na msisitizo mahsusi kusafisha akili na fikra ya Muislamu.
Juhudi kubwa sana zimefanywa na Seminari kuweka katika machapisho yake yale ambayo yanaaminika na thabiti kweli katika Uislamu.

Unaombwa kwa ukarimu kukisoma kitabu hiki kwa moyo ambao umekusudiwa. Pia unaombwa uwe huru kuwasilisha kwetu maoni yako ambayo yatathaminiwa sana kuhusu uenezi wetu.

Kutangaza ujumbe wa Uislamu ni kazi inayotaka ushirikiano wa watu wote. Seminari inakukaribisha katika kazi hii ikikubaliana kwa furaha na Aya ya Quran Tukufu.

قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُمْ بِوَاحِدَةٍ ۖ أَنْ تَقُومُوا لِلَّهِ مَثْنَىٰ وَفُرَادَىٰ{46}

“Sema; Mimi ninakunasihini kwa jambo moja tu ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja.” (34:46).

Mwenyezi Mungu na akurehemu.
Wako katikaUislamu.