Sura Ya Kumi Na Mbili

Abdul Hamid wa Misri na Allamah Abdullah Subaiti wameandika kwamba Abu Dharr alikaa Madina baada ya kifo cha Umar. Aliona kwamba Uthman alikuwa anawapendelea Bani Umayyah ambao mvuto wao ulipenya kwa kina kirefu katika serikali ya Kiislamu ambapo ilikwisha pata utukufu wa himaya. Watu waliendekeza ufahari na maonesho na waliishi maisha ya anasa sana. Watu walipendelea zaidi pato la dunia.

Aliona kwamba masahaba wengi walibadilika kabisa. Zubayr, Talha na Abdul Rahman bin Auf (wakawa wamepatana na serikali) walinunua ardhi na nyumba! Sad bin Abi Waqqas alikuwa na mawe magumu yaliyo kongomewa kwenye ikulu yake, aliinyanyua sana, akapanua na akajenga minara juu yake.

Kwa hiyo, Abu Dharr alisimama na akajitokeza wazi wazi. Hangevunjwa moyo na kamanda au Khalifa yeyote. Alianza kuwaita watu na kuwataka washikilia maadili na kumshambulia Uthman katika hotuba zake.

Siku moja alitambua kwamba Uthman alimpa moja ya tano ya ushuru kutoka Afrika Marwan bin Hakam, dinari 300,000 alimpa Harith bin al-As, Zayd bin Thabit alimpa dinari 100, 000, Abdullah bin Ali Sarah kaka yeke wa kuchangia ziwa, alimpa sehemu kubwa sana isiyo na idadi ngawira kutoka Afrika, na ardhi ya Fadak iliyoporwa kwa Fatimah alimpa Marwan alianza kukariri aya hii msikitini:

وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيم{34}

“Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia za Mwenyezi Mungu.” (Quran Tukufu, 9:34).

Marwan akatambua kwamba Abu Dharr alimshambulia yeye na Uthman, akalalamika kwa Uthman ambaye alimuagiza mtumishi wake amwite Abu Dharr aende kwake. Abu Dharr alikwenda kwake. Uthman alipomuona akasema, “Abu Dharr! Acha hayo ambayo nayasikia, vinginevyo hutamuona mtu yeyote aliye na madhara kwako isipokuwa mimi.” Abu Dharr akasema, “Ewe kamanda! Umesikia ninasema nini?” Uthman akasema, “Nimetambua kwamba unawachochea watu dhidi yangu.”

Abu Dharr aliuliza, “Kwa vipi?” Uthman alisema, “Unakariri aya ‘Tangaza . . . mateso machungu . . . ndani ya msikiti.” Abu Dharr akasema, “Ewe kamanda! Unanikataza mimi nisikariri kitabu cha Mwenyezi Mungu na nisifichue dosari za wale ambao wameacha amri za Mwenyezi Mungu! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, siwezi kumkosea Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Uthman. Hasira ya Uthman ni bora zaidi kwangu kuliko hasira ya Mwenyezi Mungu.”

Aliposikia hivi Uthman alimkunjia uso Abu Dharr lakini hakuweza kuamua ajibu vipi maneno ya Abu Dharr. Kwa hiyo, hakusema kitu na akanyamaza kwa muda fulani. Abu Dharr alisimama na akaondoka hapo, akiwa na azimio madhubuti la kuwakosoa wale ambao walikuwa wanafanya kinyume na amri za Mwenyezi Mungu kuliko kipindi chochote kile.

Abu Dharr alimshambulia Uthman mara nyingi zaidi. Kwa hiyo alikasirika sana na alingojea fursa ijitokeze amfukuze Abu Dharr aende uhamishoni. Siku moja alipata nafasi na akaitumia.

Kwa mujibu wa Bin Wazir mwandishi wa Tarikh Yaqubi, watu walimwambia Uthman kwamba Abu Dharr Ghifari alimdhihaki yeye msikiti na alitoa hotuba kwenye lango la msikiti ifuatayo:

“Enyi watu! Yule anayenijua mimi ananijua mimi, lakini yule ambaye hanijui mimi, ambaye hanitambui ajue kwamba mimi ni Abu Dharr Ghifari. Jina langu ni Jundab bin Junadah Rabazi.

Mwenyezi Mungu alimnyanyua Adam, Nuh, uzao wa Ibrahim na watoto wa Imrani, miongoni mwa watu wa duniani. Mtume Muhammad ni mrithi wa ujuzi wa Adam na maadili yote ambayo yaliwabainisha Mitume, na Ali bin Abi Twalib ni mrithi wa Mtume na mrithi wa ujuzi wake.

“Enyi watu mliokanganyikiwa! Endapo baada ya Mtume wenu mlimpenda yule ambaye Mwenyezi Mungu amempenda na alimweka nyuma yule ambaye Mwenyezi Mungu alimweka nyuma na amaeuwekea mipaka utawala na urithi miongoni mwa Ahlul –Bait, mungepata neema zisizo na hesabu kutoka juu ya vichwa vyenu na kutoka chini ya miguu yenu na hakuna rafiki yake Mwenyezi Mungu angekuwa masikini na fukara, na hakuna sehemu ya wajibu wa Dini ingepotezwa, na hakuna watu wawili ambao wangepambana kwa sababu ya amri ya Mungu kwa sababu wangepata taarifa kuhusu amri hiyo kwenye Kitabu cha Mungu na Sunna za Mtume, kwa mujibu wa Ahlul-Bait kuhusu Mtume wao.

Lakini kwa kuwa mmekusudia kufanya yale ambayo hamkufanya, lazima mtapata adhabu kwa sababu ya maovu yenu, na haikuchukua muda mrefu kabla ya hao ambao wamefanya uovu watajua watarudi kwa nani.”

Pia imeandikwa kwenye kitabu hicho hicho kwamba Uthman pia alipata taarifa kwamba alifanya mabadiliko ya Sunna za Mtukufu Mtume na Sunna za Abu Bakr na Umar kwenye msingi ambapo ndoto ya Ukhalifa wake ulitokeza, na kwamba Abu Dharr aliweka lalamiko hilo mbele ya Umma. Uthman aliposikia mambo haya, alimpeleka kwa Muawiyah, gavana wa Syria. Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, tukio hili lilitokea mwaka wa 30. A.H.

Wasomi wanasema kwamba kwa kuwa Abu Dharr aliendelea kumkosoa Uthman kwa matendo yake ambayo yalikiuka sheria za dini, Uthman alimwekea mipaka mikali. Uthman aliagiza kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kuzungumza na Abu Dharr au kwenda naye au kukaa naye. Mikutano iliitishwa mara kwa mara kutangaza agizo hili.

Kwa mujibu wa maelezo ya Allamah Majlis na Allamah Subaiti, Ahnaf bin Qays mara nyingi alikuwa na mazoea ya kwenda msikitini na kuketi humo siku moja aliomba kwa Mwenyezi Mungu; “Ee Mola! Nibadilishie kutokuchangamana kwangu na watu niwe na upendo na upweke wangu na watu wa kuwa nao na nipe rafiki anayefaa asiye na mfano.”

Baada ya kumaliza Swala hii alimuona mtu amekaa na kufanya ibada kwenye pembe ya msikiti. Alinyanyuka kutoka alipoketi na akamwendea mtu huyo na kuketi karibu naye. Halafu akasema, “Wewe ni nani na jina lako ni nani?” Akajibu, “Jundab bin Junadah.” Aliposikia hivi akasema, Mwenyezi Mungu mkubwa! Mwenyezi Mungu Mkubwa.”

Abu Dharr akasema, “Kwa nini ulikariri Takbira?” Akajibu, “Nilipoingia msikitini leo nilimwomba Mwenyezi Mungu anipe rafiki mzuri sana. Ametimiza matakwa yangu haraka sana na amenipa mimi heshima ya kukutana na wewe.”

Abu Dharr akasema, “Ninamwita Mwenyezi Mungu, zaidi yako, kumtukuza Yeye kwa sababu niliamriwa anayefaa. Ewe binadamu! Nisikilize mimi. Mtukufu Mtume ameniambia kwamba wewe na mimi tutakuwa sehemu ya juu sana na tutabaki hapo hadi watu wote wamefanyiwa hesabu.”

Abu Dharr aliendelea kusema; “Ewe mja wa Mwenyezi Mungu! Kaa mbali na mimi vinginevyo utapata matatizo.” Akauliza, “Vipi hivyo rafiki?” Abu Dharr alimjibu, “Uthman bin Affan amenikataza nisikae na watu na ameagiza kwamba yeyote atakayekutana na mimi na kuzungumza na mimi ataadhibiwa.” (Hayatul Qulub, cha Allamah Majlis Juzu ya 2, na Abu Dharr bin Al-Ghifari, cha Allamah Subaiti).

Kwa ufupi, Uthman alikasirishwa na ukweli wa Abu Dharr. Naye aliendelea na kazi yake licha ya kuwekewa mipaka; na Uthman alipata taarifa kama kawaida. Hatimaye, alipochoshwa na Abu Dharr aliamua kumpeleka uhamishoni Syria.