Sura Ya Nane

Masimulizi ya hadithi ni kitu chenye muhimu mkubwa. Wala si kila mtu anaruhusiwa kusimulia, ama kusikiliza simulizi zao. Ujuzi wa wahadithi ndio kipimo chake. Abu Dharr ni mmojawapo wa wasimulizi wa kuaminika, kutegemewa na wakweli ambao simulizi zao hazitiliwi shaka au kukataliwa. Amekuwa na Mtukufu Mtume kwa muda mrefu sana wa uhai wake. Kwa maelezo yake ni mengi sana miongoni mwa hayo, machache yameandikwa hapa.

Kuhusu Aya za Qurani Tukufu: Enyi mliamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, Mjumbe wake na “Ulil amr-i minkum,” Imamu Fakuddin Razi ametoa maelezo kwenye Tafsirul Kabir kwamba Aya hiyo inawazungumzia wale wasiokosea na Saiyid Ali Hamadani ameitaja katika Mawaddatul Kubra kwamba inawahusu wenye utakaso (Maimamu)Kumi na Wawili.

Lakini inahitaji kuthibitishwa na masahaba wa Mtume wenye kuheshimika kwamba Mtume mwenyewe alisimulia hadithi hiyo. Abu Dharr anasimulia kutoka kwa Mtume kwamba aya iliyotajwa hapo juu ilipofunuliwa, alimwomba Mtukufu Mtume amwambie majina ya Waku wa mambo ‘Ulil Amr. Aliwataja maimamu kumi na mbili. Baada ya kuwataja majina, Abu Dharr anatoa maelezo kwa ufupi kwamba mteule wa kwanza ni Ali na wa mwisho ni Imamu Mahdi.
(Yanabiul Mawaddah, Shaykh Sulayman Qandozy al-Hanafi na Riuzatul Ahbab).

Abu Ishaq Thalabi ameandika kwenye maelezo yake: “Siku moja Bin Abbas alikuwa anasimulia hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w) alipokuwa ameketi karibu na kisima cha Zamzam ambapo mtu mmoja aliyefunika uso wake alikuja hapo. Bin Abbas alinyamaza kwa muda. Mtu huyo alianza kusimulia hadithi ya Mtume Bin Abbas akasema, “Ewe mtu! Nina kuuliza katika jina la Mwenyezi Mungu uniambie kwa kweli wewe ni nani?”

Alifunua uso wake na akasema, “Enyi watu! Yule anayenijua mimi ananijua mimi, lakini yule asiyenijua mimi, anatakiwa anitambue kwamba mimi ni Abu Dharr Ghifari. Nimesikia kutoka kwa Mtukufu Mtume kwa masikio haya mawili ambayo yanaweza kupata maradhi na kuwa kiziwi kama sikukosea, na nimeona kwa macho haya mawili ambayo yanaweza kupofuka endapo mtasema uwongo kwamba Mtume alisema kuhusu Ali kwamba ni kiongozi wa watu waadilifu na muuaji wa watenda maovu. Mtu aliyemsaidia yeye alipata ushindi na yule aliye mtelekeza yeye naye alitupwa.”

Kufuatana na simulizi ya Abu Dharr Ghifari, Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Ali ni lango la ujuzi wangu mwongozo wa wafuasi wangu wa lengo lililosababisha nitumwe. Kumpenda yeye ni imani na kumfanyia uadui yeye ni unafiki na kuwa rafiki yake ni ibada.” (Arjahul Matalib uk. 604 kwa mamlaka ya Dailami).

Kwa mujibu wa simulizi ya Abu Dharr, Mtume alisema: “Mtu akiniheshimu mimi, anamheshimu Mwenyezi Mungu. Asiyeniheshimu mimi, hamheshimu Mwenyezi mungu.

Mtu anayemheshimu Ali, ananiheshimu mimi, na yule asiyemheshimu Ali haniheshimu Mimi.” (Arjahul Matalib Uk 606, kwa mamlaka ya Hakim).

Abu Dharr anasema; “Tulikuwa tunawatambua wanafiki kwa vitu vitatu: Kwanza kwa kumkana Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, mbili kwa kuacha kusali, na tatu kwa chuki yake dhidi ya Ali.” (Arjahul Matalib uk. 608 kwa mamlaka ya bin Shazan).

Ipo hadith ambayo imesimuliwa na Abu Dharr, kwamba Mtume alisema, “Ali ni lango la ujuzi wangu. Yeye ni msimulizi wa mambo hayo ambayo yamesababisha niteuliwe. Kumpenda Ali ni imani na kumchukia ni unafiki, na kumwangalia yeye ni ibada.”

Bin Abd al-Barr ameandika kwenye Istiab kwamba masahaba wengi wamesimulia hadithi hii ya Mtume: “Ewe Ali! Hapana yeyote atakaye kuwa rafiki yako isipokuwa muumini, na hapana yeyote atakayekuwa adui yako isipokuwa mnafiki.”
(Arjahul Matalid uk. 609 kwa mamlaka ya Dailami).

Abu Dharr amemnukuu Umm Salamah kwa kusema kwamba alimsikia Mtukufu anasema; “Ali yu mkweli na ukweli umo kwa Ali na Ali na ukweli hawatatengana hadi watakapofika kwenye Haudhi ya Neema (Arjahul Matalib uk. 699 kwa mamlaka ya Bin Marduyah)

Allmah Subaiti ameandika: “Abu Dharr amesema kwamba Mtume alimwambia yeye “Mtu anaye kubali imani kwa uaminifu huuweka moyo wake katika hali safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, husema ukweli, huwa makini, anakuwa na tabia njema, hutumia masikio yake kusikiliza mambo mazuri, na hutumia macho yake kuona vitu vinavyostahili, atapata ukombozi.”

Abu Dharr anasema kwamba Mtume amesema: “Wafuasi wangu hawataneemeshwa endapo watafuturu kabla ya muda, na kuchelewa kula daku kabla ya alfajiri (muda wa kuanza kufunga wakati wa mwezi wa ramadhani).”

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume anasema: “Furaha yangu ni kwamba dhahabu igawiwe kama sadaka hata kama ingekuwa kubwa kama Mlima Uhud.”
(Tafsir Bin Kathir uk. 61).

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume amesema: “Ewe Ali! Mwenyezi Mungu ametufanya mimi na wewe kuwa mti mmoja. Mimi ni mizizi ya mti huo na wewe ni tawi lake. Mwenyezi Mungu atamtupa mtu Jahananu kwa kutanguliza uso wake, kama akikata Tawi Lake.” Aliendelea kusema, “Ali ni kiongozi wa Waislamu na Imamu wa wacha Mungu. Atawaua watakaovunja ahadi ya utiiifu kwake (watu wa Jamal), walio tengwa na jamii (makhawariji) na wakanushaji.” (Tafsir bin Kathir uk. 61).

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume amesema; “Ali kwangu ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa tofauti moja tu kwamba hapatakuwepo na Mtume badala yangu.” Hadithi hii imenukuliwa na masahaba wengine wengi, miongoni mwao wakiwemo Umar bin Khatab, Sa’d bin Abi Waqqas, Abu Hurayrah, Abdullah bin Mas’oud, Abdallah bin Abbas, Jabir bin Abdullah, Abu Said Khidri, Jabir bin Samrah, Malik bin Harith, Bara bin Azib, Zayd bin Arqam, Anas bin Malik, Abu Ayyub Al-Ansari, Aqil bin Abi Talib na kadhalika (Arjahul Matalib).

Allamah Abdul Mu’min Shablanji ameandika kwenye kitabu chake:‘Nurul Absar’ kwamba, Abu Dharr, ananukuu kutoka kwa Mtume ambaye alisema: “Kitendo kizuri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kumpenda yeye na kutofanya chochote kinyume na Ridhaa Yake..”

Abu Dharr anamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w) akisema: “Unapokuwa na urafiki na mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mfahamishe.”

Abu Dharr anasimulia kwamba Mtukufu Mtume anasema; “Mtu anapokasirika, kama amesimama, ni vema aketi chini na endapo hasira haipungui, alale chini.” (Nurul Absar, Uk. 29).

Abu Dharr ananukuu hadithi ya Mtume kwamba Mwenyezi Mungu humpenda mtu anaye vumilia anapotendewa mabaya na jirani yake (Nurul Absar, uk. 32).

Abu Dharr anasema kwamba Mtume (s.aw.) ameagiza uchaji Mungu na kujinyima na alituomba tulinde dhamana, tusipite tunaomba kwa mtu yeyote, tusivunje uhusiano wa kimapenzi uliopo baina ya watu wawili, kumtendea wema mtu anayekutendea ubaya, na kumuogopa Mwenyezi Mungu kila mara katika jambo la wazi na siri (Nurul Absar, uk. 33).

Abu Dharr anasimulia hadith ya Mtume hivi: “Mwenyezi Mungu alifananisha Ahlul Bait na Safina ya Nuhu (Safinatu Nuh) kwa wafuasi wangu. Yeyote aliyepanda humo, aliokoka na yeyote ambaye hakupanda alikufa maji, yaani kwa usemi mwingine alikengeuka.

Pia Ahlul Bait wangu, wapo kama mlango wa kwendea toba (Hittab) kwa wafuasi wangu. Kuhusu wana wa Uyahudi ambao Mwenyezi Mungu aliwaambia kwamba mtu aliyeingia kupitia mlangoni, ataokoka kutokana na mateso ya dunia na Akhera. Vivyo hivyo, yeyote yule kutoka miongoni mwa wafuasi wangu akifuata njia ya Ahlul-Bait wangu na anaendelea kuwa imara katika kuwafuata, ataokolewa katika Siku ya Hesabu.” (Ainul Hayat).

Ali bin Shahab Hamadani anamnukuu Abu Dharr ambaye anasema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume anasema; “Ewe Abu Dharr! Ali ni yeye ndiye atakayezigawanya Pepo na Jahanamu. Ewe Abu Dharr! Hakuna hata malaika moja aliyeweza kupata heshima ya kugawa Pepo kutoka kwenye Jahamanu. Tazama! Pepo ipo pale kwa ajili ya wanao muunga mkono yeye na amepewa ndugu kama mimi ambapo hakuna ndugu wa mtu yeyote kama mimi.”

Abu Dharr anamnuku Mtukufu Mtume akisema; “Mwenyezi Mungu ameimarisha Uislamu kupitia kwa Ali, Ali anatokana na mimi na mimi ninatokana na Ali, na Aya hii,

أَفَمَنْ كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِنْهُ وَمِنْ قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُولَٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۚ وَمَنْ يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ ۚ فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِنْهُ ۚ إِنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ{71}

“Basi mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake Mlezi, inayofuatwa na shahidi anaye toka kwake na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa mwongozi na rehema …” (11:17).
Imeteremshwa kuhusu yeye (Ali) mimi ninao uthibitisho katika Aya hii na Ali ni shahidi yangu” (Muwaddatul Qurba, uk. 78)

Kwa mujibu wa Abu Dharr, Mtume alimwambia Ali, “Ewe Ali! Mtu anayenitii mimi, anamtii Mwenyezi Mungu na mtu anayekutii wewe, ananitii mimi, na mtu asiyenitii mimi hamtii Mwenyezi na mtu asiyekutii wewe, hanitii mimi.” (Muwaddatul Qurba uk. 78 na Yanabiul Mawaddah, Shaykh Sulayman Qandozy).

Abu Dharr anasema kwamba siku moja alipokuwa kwenye Uwanja wa makaburi wa Baqi’ (Madina) na Mtume (s.a.w), ambapo alisema, “Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye anaoudhibiti wa maisha yangu kwamba yupo mtu miongoni mwenu ambaye atapigana kwa ajili ya fasiri iliyo sahihi ya Quran Tukufu, kwa namna ile ile niliyopigana mimi na wanao abudu miungu wengi wakati wa ufunuo wa Qurani, ingawa watakuwa wanakariri mfumo ya imani (Hapana Mungu ila Mwenyezi Mungu). Ambapo yeye (Ali) atapigana nao watu wataona si sahihi na watamkosoa rafiki ya Mwenyezi Mungu (yaani Ali) na watamkasirikia kwa sababu ya vita hii kama Mtume Musa alivyomkasirikia Khidhr kwa sababu ya kutoboa mashua, kumuua mtoto na kujenga ukuta, ingawa kutoboa mashua, kumuua mtoto na kujenga ukuta ni matukio yaliyotekelezwa kufuatana na amri ya Mwenyezi Mungu.” (Arjahul Matalib uk. 31).

Muhammad bin Yusuf Kanji Shafii amemnukuu Abu Dharr akisema kwamba Mtume alisema, Bendera ya Ali bin Abi Talib, kiongozi wa waumini, kiongozi mkuu wa wenye nyuso zing’arazo na mrithi wangu itanifikia mimi kwenye Haudhi ya Neema (kifay tut Talib).

Abu Dharr anasema kwamba alimuuliza Mtume, “Ni msikiti gani wa kwanza kujengwa hapa duniani? “ Akajibu, “Msikiti wa al-Haram ” Akasema, “Na baada ya huo?” Akajibu, “Msikiti wa Bayt al-Maqdis (Yerusalemu)” Halafu akasema, “Palikuwepo urefu gani wa kipindi?” Mtume alijibu, “Miaka arobaini.” (Tajrid Bukhari).

Imamu Bukhari amemnukuu Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume alisema, “Endapo kwa makusudi mtu anajihusisha na mtu mwingine kwamba ni baba yake ambapo sivyo, mtu huyo si muumini, na mtu, ambaye anajionesha kwamba yeye ni mtu wa jamii ambamo hana wazazi. Lazima ajitayarishe kufanya Jahanamu kuwa masikani yake.” (Tajrid Bukhari).