Kitabu hiki kinazungumzia juu ya hitilafu zilizotokea juu ya maneno yanayosomwa katika Adhana. baadhi ya wanachuoni wanasema kwamba kuna maneno yaliyoongezwa, na wengine wanasema kuna baadhi ya maneno yaliyoondolewa. Ili kujua ukweli wa asili ya Adhana na maneno yake.

Mwanachuoni Sheikh Jafar Subhani amefanya utafiti juu ya sula hili na kuonesha kwa uwazi na pasina shaka yoyote juu ya asili ya Adhana na maneno yake.
Mwanachuoni huyu mtafiti ametumia vyanzo halisi na sahihi katika kulifikia lengo lake hili. vyanzo hivyo si vingine bali ni Qur.an na Sunna, pamoja na matukio ya kweli ya kihistoria, akili, mantiki na ilmu.