Aya 31 – 46: Basi Makusudio Yenu Ni Nini Enyi Mliotumwa?
قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ {31}
قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُجْرِمِينَ {32}
لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِنْ طِينٍ {33}
مُسَوَّمَةً عِنْدَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ {34}
فَأَخْرَجْنَا مَنْ كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ {35}
فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِنَ الْمُسْلِمِينَ {36}
وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَةً لِلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الْأَلِيمَ {37}
وَفِي مُوسَىٰ إِذْ أَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَانٍ مُبِينٍ {38}
فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ {39}
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ {40}
وَفِي عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ {41}
مَا تَذَرُ مِنْ شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ {42}
وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّىٰ حِينٍ {43}
فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنْظُرُونَ {44}
فَمَا اسْتَطَاعُوا مِنْ قِيَامٍ وَمَا كَانُوا مُنْتَصِرِينَ {45}
وَقَوْمَ نُوحٍ مِنْ قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ {46}
Maana
Akasema: Basi makusudio yenu ni nini, enyi mliotumwa?
Ibrahim (a.s.) anawauliza wageni wake baada ya kuwajua ni akina nani, kuwa je, wanakwenda wapi na wanataka nini?
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu; yaani kaumu ya Lut. Walikuwa ni wakosefu waliopituka mipaka, kwani walikuwa wakiwaendea wanaume kwa matamanio badala ya wanawake.
Tuwatupie mawe ya udongo, yaliyotiwa alama kutoka kwa Mola wako kwa ajili ya wanaopituka mipaka.
Tutawaangamiza kwa mawe yaliyotiwa alama yanayotokana na udongo mkavu aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa wanaopituka mipaka katika ukafiri dhulma na ufisadi.
Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walioamini ili yasiwasibu yale yatakayowasibu waliopituka mipaka.
Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! Hiyo ni nyumba ya Lut, ukimtoa mkewe aliyekuwa katika walioangamia.
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanaoiogopa adhabu chungu. Yaani humo mjini mwa watu wa Lut. Makusudio ya ishara ni athari zinazojulisha kuangamia kwao na adhabua yao, ili iwe ni funzo kwa mwenye kutaamali.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7: 80-84) na Juz. 12 (11: 77-83).
Na katika habari za Musa, tulipomtuma kwa Firauni na hoja wazi.
Mwenyezi Mungu alimtuma Musa kwa Firauni akiwa na miujiza ya kutosheleza kumkemea Firauni na upotevu wake, Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake.
Alipuuza kwa kughurika na jeshi lake na utawala wake.
Na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!
Kwa nini Musa ni mchawi au mwendawazimu katika mantiki ya Musa? Ni kwa vile alimwambia wewe si Mungu wa kuabudiwa na akamhadharisha na dhulma na kupituka mipaka.
Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.
Alipituka mipaka na akasema: Mimi ndiye Mola wenu mkubwa, ikawa mwisho wake ni kuangamia na kulaumiwa.
Katika ziada ya maneno ni kuwa huko nyuma tuliashiria sababu za kukaririka. Katika Juz. 16 (20:9-16), tulitaja sababu za kukaririka kisa cha Musa. Ama hapa tunasema: “Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.”
Na katika habari za A’di tulipowapelekea upepo wa kukata uzazi.
Mwenyezi Mungu aliwaangamiza A’di na kaumu ya Hud kwa upepo unaovuma, unaobomoa kila kitu. Haukuacha chochote ulichokifikia ila ulikifanya kama unga. Kila unachokipitia unakivunja na kukipondaponda.
Kisa cha Hud na watu wake kimetangulia katika Juz. 8 (7:73-79) na Juz. 12 (11:50-60).
Na katika habari za Thamudi walipoambiwa: Stareheni kwa muda mdogo tu.
Thamud ni watu wa Swaleh. Aya hii inaashiria yaliyoelezwa katika Juz. 12 (11:65): “Basi (Swaleh) akasema: Stareheni katika mji wenu kwa siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyokadhibishwa.”
Basi wakaasi amri ya Mola wao, mara kimondo kikawanyakua nao wanaona.
Walimwasi Mwenyezi Mungu na Mtume, ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawateremshia adhabu kutoka mbinguni.
Walipoona zikipomoka nguvu zao, basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
وَإِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِقَوْمٍ سُوءًا فَلَا مَرَدَّ لَهُ ۚ وَمَا لَهُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَالٍ {11}
Kisa cha Swaleh kimetangulia katika Juz. 8 (7: 73 – 79) na katika Juz. 12 (11: 61-68).
Na kaumu ya Nuh hapo mbele Mwenyezi Mungu aliwaangamiza kwa dhambi zao.
Hakika hao walikuwa watu mafasiki wakifanya mambo ya kuangamiza na kuvunja miko ya haramu. Kimetangulia kisa cha Nuh, Juz. 8 (7: 59 – 64) Juz. 12 (11: 25-49).
وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ {47}
وَالْأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ {48}
وَمِنْ كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ {49}
فَفِرُّوا إِلَى اللَّهِ ۖ إِنِّي لَكُمْ مِنْهُ نَذِيرٌ مُبِينٌ {50}
وَلَا تَجْعَلُوا مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ ۖ إِنِّي لَكُمْ مِنْهُ نَذِيرٌ مُبِينٌ {51}
كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ مِنْ رَسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ {52}
أَتَوَاصَوْا بِهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ {53}
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنْتَ بِمَلُومٍ {54}
وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنْفَعُ الْمُؤْمِنِينَ {55}
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ {56}
مَا أُرِيدُ مِنْهُمْ مِنْ رِزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَنْ يُطْعِمُونِ {57}
إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ {58}
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبًا مِثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ {59}
فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ {60}