Aya 33 – 42 : Lut
Maana
Watu wa Lut waliwakadhibisha waonyaji, sawa na walivyokadhibisha watu wa Nuh, A’di Thamud na wengineo. Siri yao ni moja tu, mapambano ya haki na batili na uadilfu na dhulma. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akabainisha aina ya adhabu iliyowashukia watu wa Lut kwa kusema:
Hakika tuliwapelekea kimbunga cha vijiwe.
Yaani aliwatupia vijiwe vilivyochukuliwa na upepo. Vijiwe hivi ndivyo alivyovitaja Mwenyezi Mungu katika Juzuu hii tuliyonayo (51:33).
Isipokuwa wafuasi wa Lut. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.
Mwenyezi Mungu alimwokoa Lut na wale waliokuwa pamoja naye, pale alipowatoa usiku kutoka kwenye kijiji ambacho watu wake wamekuwa madhalimu.
Kwa neema inayotoka kwetu. Hivyo ndivyo tunavyomlipa anayeshukuru.
Mwenyezi Mungu alimwadhibu aliyeasi na akamneemesha aliyetii kwa kutumia misingi ya uadilifu. Lakini Razi anasema: “Hata kama wangeliaangamizwa watu wa Lut pia ingelikuwa ni uadilifu.”
Mwenyezi Mungu ndiye mkweli zaidi wa mazungumzo; naye ndiye aliyesema:
وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ {115}
Juz. 8 (6:115).
Yaani uadilifu ni ule uliokwishatimia; vinginevyo ni dhulma.
Na hakika yeye aliwaonya mkamato wetu; lakini waliyatilia shaka hayo maonyo.
Lut aliwahadharisha na adhabu ya Mwenyezi Mungu, lakini wakatia shaka na wakadharau; bali hata walitoa vitisho na:
قَالُوا لَئِنْ لَمْ تَنْتَهِ يَا لُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمُخْرَجِينَ {167}
Juz. 19 (26:167).
Na walimtaka awape wageni wake.
Walisikia kuwa kuna wageni kwa Lut, kwa hiyo wakaenda kwake haraka na wakamwambia kwa ufidhuli: tupatie wageni wako tuwafanyie uchafu.
Tukayapofua macho yao.
Yaani Mwenyezi Mungu aliyatia upofu macho yao wasiweze kuwaona, kisha akawapelekea adhabu na akawaambia: Basi onjeni adhabu na maonyo yangu ambayo miliyatilia shaka na kuyadharau
Na iliwafikia asubuhi adhabu ya kuendelea.
Iliwafikia adhabu asubuhi, ikaendela hadi ikawamaliza wote.
Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!
Haya ameyasema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) baada ya adhabu ya kupofuka, kisha akayakariri baada ya adhabu ya mawe
Na hakika tumeifanya Qur’an iwe nyepesi kuikumbuka. Basi je yupo anayekumbuka?
Ameikariri Aya hii, ambaye imetukuka hikima yake, mara nne: Ya kwanza ni baada ya kuashiria kisa cha Nuh, ya pili ni baada ya kisa cha Hud, ya tatu baada ya kisa cha Swaleh na ya nne ni hapa baada ya kisa cha Lut.
Lengo ni kupata mazingatio na mafunzo katika kila moja ya visa hivi vine. Kwa sababu ni tosha kabisa katika waadhi na ukumbusho.
Kisa cha Lut kimekwisha tangulia katika sura ya 11, katika Juz.12, na nyinginezo.
Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
Mfano wake ni Aya isemayo:
ثُمَّ بَعَثْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ {103}
Walizikadhibisha Ishara zetu zote; nazo zilikuwa tisa; kama anavyosema Mwenyezi Mungu:
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ تِسْعَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ {101}
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amezitaja tano pale aliposema:
فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُفَصَّلَاتٍ {133}
Nyingine nne amezitaja katika Aya mbalimbali; nazo ni mkono, fimbo, kufunguka kifundo katika ulimi wa Musa na kupasuka bahari.
Tukawashika mshiko wa Mwenye nguvu Mwenye uweza.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwangamiza Firauni na watu wake majini na hapo mwanzo alikuwa akiwaambia watu wake: Mimi ndiye Mola wenu mkuu. Basi Mwenyezi Mungu akamuonjesha adhabu ya hizaya ya dunia na adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi.
أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِنْ أُولَٰئِكُمْ أَمْ لَكُمْ بَرَاءَةٌ فِي الزُّبُرِ {43}
أَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيعٌ مُنْتَصِرٌ {44}
سَيُهْزَمُ الْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ الدُّبُرَ {45}
بَلِ السَّاعَةُ مَوْعِدُهُمْ وَالسَّاعَةُ أَدْهَىٰ وَأَمَرُّ {46}
إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ {47}
يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ {48}
إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ {49}
وَمَا أَمْرُنَا إِلَّا وَاحِدَةٌ كَلَمْحٍ بِالْبَصَرِ {50}
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ {51}
وَكُلُّ شَيْءٍ فَعَلُوهُ فِي الزُّبُرِ {52}
وَكُلُّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ مُسْتَطَرٌ {53}
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَهَرٍ {54}
فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِنْدَ مَلِيكٍ مُقْتَدِرٍ {55}