read

Aya 43 – 55: Kila Kitu Tumekiumba Kwa Kipimo

Maana

Je, Makafiri wenu ni bora kuliko hao?

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad (s.a.w.). Hao ni watu wa uma zili- zotangulia walioangamia kwa sababu ya kufuru na inadi yao. Katika Aya zilizotangulia Mwenyezi Mungu ametaja aina za adhabu zilizowapata.

Maana ni kuwa nyinyi sio bora zaidi ya tuliowaangamiza; bali nyinyi ni waovu zaidi na wenye uasi zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Je, mmejiaminisha yasiwapate yale yaliyowapata wenzenu au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi mtaachwa? Je, Mwenyezi Mungu ameteremsha katika kitabu chochote miongoni mwa vitabu vyake kuwa nyinyi mtasalimika na adhabu yake?

Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda?

Hivi nyinyi mnadai kwa ni kundi kubwa lilisiloshindwa?

Wingi wao huu utashindwa, na watasukumwa nyuma.

Iliposhuka Aya hii washirikina ndio waliokuwa na nguvu, kwa vile walikuwa wengi. Ama waislamu walikuwa ni mmoja mmoja wadhaifu. Mshirikina yeyote alikuwa na uwezo wa kumuudhi Mwislamu.

Lakini hazikupita siku na mambo yakageuka, washirikina wakasukumwa nyuma, Uislamu na waislamu wakawa juu, na ikabainika kwa ukaribu na umbali kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Wingi wao huu utashindwa,’ kuwa ni kweli. Hii peke yake ni ubainifu mkataa kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anatamka kupitia kwenye ulimi wa Mtume wake mtukufu (s.a.w.).

Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito sana na chungu zaidi.

Neno ‘yao,’ linawarudia wote, kuanzia kaumu ya Nuh mpaka makafiri wa Kiarabu ambao walimkadhibisha Muhammad (s.a.w.). Maana ni kuwa kila adhabu iliyowapata makafiri duniani, si chochote kulinganisha na adhabu ya Akhera. Kila balaa isyokuwa Moto hiyo ni salama.

Hakika wakosefu wamo katika upotofu na mioto. Siku watakapokokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!

Hii ni tafsiri na ubainifu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na Saa hiyo ni nzito sana na chungu zaidi.’ Watu wa motoni hawatatosheka na vituko vyake tu, bali Malaika wa adhabu watawahamishia kwenye adhabu mbalimbali; kama vile kuvutwa kifudifudi, makomeo ya chuma na mengineyo yasiyoelezeka.

Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.

Aya ya pili inasema:

وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا {2}

“Na ameumba kila kitu na akakikadiria kipimo.” Juz. 18 (25:2).

Ya tatu inasema:

وَكُلُّ شَيْءٍ عِنْدَهُ بِمِقْدَارٍ {8}

“Na kila kitu kwake ni kwa kipimo.” Juz. 13 (13:8).

Ya nne:

الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ {2}

وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ {3}

“Ambaye ameumba akalinganisha sawa na Ambaye amekadiria na akaongoza.” (87:2-3).

Na kuna Aya nyinginezo nyingi zinazofamisha kuwa hakuna kitu chochte kilichopo ila kimekadiriwa kwa kipimo maalum na sifa zisizozidi wala kupungua vile inavyotakikana na kwamba kila kilichomo ndani yake kitakuwa kimepangwa kwa mpangilio mzuri na kuweka mahali panapolingana na wadhifa na umuhimu wake.

Tukitafuta kilichosababisha hivyo kinachokubalika kiakili, hatupati isipokuwa utashi wa Mwenyezi Mungu ambao uko nyuma ya kila kitu. Anasema Conte: “Maumbile ni kama kazi ya usanii. Kuitolea dalili ya chimbuko lake ni sawa na kutolea dalili athari pale ilipotokea.”

Unaweza kuuliza: Hiwezekani kuwa nidhamu hii imetokana na kazi ya sadfa?

Jibu: Sadfa kama lilivyo jina lake, haiwezekani kukaririka. Kuyafasiri matukio kwa sadfa, itakuwa ni kukimbia. Hayo ni kwa hukumu ya akili na uhalisia. Ndio maana wakasema maulama kuwa, hakimbilii kwenye sadfa ila mwenye kushindwa.

Zaidi ya hayo, kama nadharia hii ingelikuwa sahihi basi ilimu isingelikuwa na maana kabisa. Kwa sababu ilimu ina misingi maalumu; vinginevyo itakuwa si ilimu. Kinyume na sadfa ambayo huwa haina maaudhui maalumu, na kama itakuwa na maaudhui maalum, basi itakuwa nayo siyo sadfa.

Ikiwa sadfa ni batili, basi madhehebu ya wanaosema kuwa maada ndio asilili ya kila kitu nayo yatakuwa ni batili.

Ni nani mwenye akili anayeweza kukubali kuwa ulimwengu umepatikana kwa sadfa, kila kilichomo ndani yake ikiwemo kanunui na nidhamu imepatikana kwa sadfa na maada nayo imepatikana kwa sadfa? Hapa ndio tunakuta tafsiri ya kauli ya msahiri: “Kila kitu ni ishara kwake kutambulisha umoja wake.”

Pia tafsiri ya aliyesema: “Uwezekano si zaidi ya ulivyo.” Yaani kila kitu kimewekwa mahali panaponasibiana nacho, lau kitaepuka hata kiasi cha unywele basi itabainika kasoro na upungufu.

Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.

Hiki ni kinaya cha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akitaka kukileta kitu ni kiasi cha kutaka tu, wala hahitajii wakati hata ule wa kupepesa jicho au chini yake. Ametaja kupepesa jicho kwa kiasi cha kuleta karibu maana tu.

Kwa maneno ya wanafalsafa ni kuwa mnasaba wa matakwa yake Mwenyezi Mungu kwa anachokitaka ni kama mnasaba wa kupatikana kinachopatikana.

Na bila ya shaka tumekwishawaangamiza wenzenu. Je, yupo anayekumbuka?

Katika wakati uliopita walikuweko wenzenu waliojiona kama mnavyojiona nyinyi enyi washirikina wa kiarabu; wakawakadhibisha mitume wao kama nyinyi mnavyomkadhibisha Muhammad (s.a.w.), Mwenyezi Mungu akawapondaponda kabisa. Basi chukuueni somo kwao kabla ya kuchukuliwa somo nyinyi.

Na kila kitu walichokifanya kimo vitabuni. Na kila kidogo na kikub- wa kimeandikwa.

Si kauli wala kitendo, kiwe kidogo au kikubwa kitakuwa kimethibitishwa, kwa aliyekitenda, katika ilimu ya Mwenyezi Mungu. Mwenye faida ni yule anayejihisabu kabla ya kuhisabiwa.

Hakika wenye takua watakuwa katika Mabustani na mito. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.

Wenye takua ni wale waliojiangalia na wasijiingize kwenye maangamizi kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. Wakajihisabu kwa kila dogo na kubwa, wakawa ni wenye kukurubishwa kwa Mwenyezi Mungu.