Sura Ya Hamsini Na Mbili: At-Tur
Imeshuka Makka. Ina Aya 49.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
وَالطُّورِ {1}
Naapa kwa Mlima,
وَكِتَابٍ مَسْطُورٍ {2}
Na kitabu kilichoandikwa
فِي رَقٍّ مَنْشُورٍ {3}
Katika waraka wa ngozi iliyo kunjuliwa,
وَالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ {4}
Na kwa Nyumba iliyojengwa,
وَالسَّقْفِ الْمَرْفُوعِ {5}
Na kwa sakafu iliyonyanyuliwa,
وَالْبَحْرِ الْمَسْجُورِ {6}
Na kwa bahari iliyojazwa.
إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَاقِعٌ {7}
Hakika adhabu ya Mola wako hapana shaka itatokea.
مَا لَهُ مِنْ دَافِعٍ {8}
Hapana wa kuizuia.
يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرًا {9}
Siku zitakapotikisika mbingu kwa mtikiso,
وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرًا {10}
Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.
فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ {11}
Basi ole wao siku hiyo wanaokadhibisha,
الَّذِينَ هُمْ فِي خَوْضٍ يَلْعَبُونَ {12}
Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi.
يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا {13}
Siku wataposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu.
هَٰذِهِ النَّارُ الَّتِي كُنْتُمْ بِهَا تُكَذِّبُونَ {14}
Huu ndio ule Moto mliokuwa mkiukadhibisha!
أَفَسِحْرٌ هَٰذَا أَمْ أَنْتُمْ لَا تُبْصِرُونَ {15}
Je, huu ni uchawi, au hamuoni?
اصْلَوْهَا فَاصْبِرُوا أَوْ لَا تَصْبِرُوا سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {16}
Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyokuwa mkiyatenda.