read

Sura Ya Hamsini Na Sita: Al-Waaqia

Imeshuka Makka. Ina Aya 96.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ {1}

Litakapotukia hilo Tukio.

لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ {2}

Hapana cha kukanusha kutukia kwake.

خَافِضَةٌ رَافِعَةٌ {3}

Literemshalo linyanyualo.

إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا {4}

Itakapotikiswa ardhi kwa mtikiso,

وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا {5}

Na milima itaposagwasagwa,

فَكَانَتْ هَبَاءً مُنْبَثًّا {6}

Iwe mavumbi yanayopeperushwa.

وَكُنْتُمْ أَزْوَاجًا ثَلَاثَةً {7}

Na nyinyi mtakuwa namna tatu.

فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ {8}

Basi watakuwepo wa kuume; je, ni yapi ya wa kuume?

وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ {9}

Na wa kushoto; je, ni yapi ya wa kushoto?

وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ {10}

Na waliotangulia ndio waliotangulia.

أُولَٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ {11}

Hao ndio watakaokaribishwa

فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ {12}

Katika Bustani zenye neema

ثُلَّةٌ مِنَ الْأَوَّلِينَ {13}

Fungu kubwa katika wa mwanzo,

وَقَلِيلٌ مِنَ الْآخِرِينَ {14}

Na wachache katika wa mwisho.

عَلَىٰ سُرُرٍ مَوْضُونَةٍ {15}

Watakuwa juu ya viti vya fahari vilivyodariziwa.

مُتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ {16}

Wakiviegemea wakielekeana.

يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُخَلَّدُونَ {17}

Watawazunguukia vijana wa milele.

بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِنْ مَعِينٍ {18}

Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi.

لَا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنْزِفُونَ {19}

Hawataumwa kichwa kwa hivyo wala hawataleweshwa.

وَفَاكِهَةٍ مِمَّا يَتَخَيَّرُونَ {20}

Na matunda wayapendayo,

وَلَحْمِ طَيْرٍ مِمَّا يَشْتَهُونَ {21}

Na nyama ya ndege kama wanavyotamani.

وَحُورٌ عِينٌ {22}

Na Mahurulaini.

كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ {23}

Walio kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa.

جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {24}

Ni malipo kwa waliyokuwa wakiyatenda.

لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا {25}

Humo hawatasikia upuzi wala maneno ya dhambi.

إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا {26}

Isipokuwa maneno ya Salama, Salama.