read

Aya 1-3: Aya Za Kitabu Kinachobainisha

Maana

Alif laam raa.

Umetangulia mfano wake katika mwanzo wa sura Baqara. Juz. 1 (2:1)

Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

Hizo ni ishara ya Aya za sura hii na Kitabu kinachobainisha ni Qur’ani. Mwenyezi Mungu amekisifu kuwa ni chenye kubainisha, kwa sababu kinauweka wazi utume wa Muhammad (s.a.w.) na kinadhihirisha uongofu

Hakika sisi Tumeiteremsha Qur’ani kwa kiarrabu ili mpate kutia akilini.

Maana yako ya wazi kwamba Mwenyezi Mungu ameiteremsha kwa lugha ya kiarabu ili watambue siri yake na utukufu wake, wayafahamua maana yake na wayatumie. Unaweza kuuliza: Muhammad ametumwa kwa watu wote kama inavyose-ma Qur’ani:

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا {28}

“Na hatukukutumua ila kwa watu wote uwe mbashiri na muonyaji” (34:28).

Na kuteremshwa Qur’ani kwa lugha ya kiarabu kunafahamisha kuwa yeye ni wa Waarabu tu, si wa wengine. Sasa tutazioanishaje Aya mbili hizi?
Jibu: Kwanza, kuteremshwa Qur’ani kwa Lugha ya kiarabu hakummaaanishi kuwa waarabu peke yao ndio wanaokalifiwa na hukumu zake na mafunzo yake. Qura’ni yenyewe na wale wanaoiamini wanaisadikisha Tawrat iliyoteremshiwa Musa (a.s.) na Injil iliyoteremshiwa Issa (a.s.) na lugha ya vitabu hivyo siyo lugha ya Qur’ani wala ya wale wanayoiamini.

Pili, lugha ni nyenzo na maana ndio lengo. Haiwezekani kuwa maana yahusike na kaumu fulani tu. Kwani watu wote wanaamini ukaumu wa binadamu. Kwa maneno mengine lugha inahusika na watu fulani, lakini maana yanawaenea wote, hayana kundi fulani wala jinsi fulani.

Tatu, ikiwa Mtume hatatumwa kwa lugha ya watu wake basi ataleta ujumbe kwa lugha gani na hakuna lugha inayozungumzwa na wote? Hapa ndipo inafichuka siri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ رَسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ {4}

“Na hatukumtumma Mtume yeyote ila kwa lugha ya watu wake ili apate kuwabainishia.” (14:4).

Sisi tunakusimulia simulizi nzuri sana kwa kukupa wahyi Qur’ani hii.

Makusudio ya simulizi ni habari za mitume zilizokuja katika Qur’ani Tukufu, nazo ni habari nzuri sana kutokana na mafunzo na hekima zili- zomo ndani yake.

Na hakika kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa wasio na habari.

Kwa sababu yalitokea karne zilizopita nayo hayajulikani kiujumla. Hii ni dalili mkataa kwamba ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنْتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ {52}

“Na kama hivyo tulikupa wahyi roho (Qur’ani) kwa amri yetu. Hukuwa ukijua Kitabu ni nini wala imani.” (42:52).

Mwenye kuisoma vizuri Qur’ani, akayazingatia maana yake ataishia kuamini kwamba hakuna anayeweza kujua yote isipokuwa yule ambaye kila kitu amekizunguka kwa ujuzi wake.”

إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ {4}

Yusuf alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja na jua na mwezi nimeota zikinisujudia.

قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنْسَانِ عَدُوٌّ مُبِينٌ {5}

Akasema: Ewe mwanagu! Usiwasimulie ndugu zako ndoto yako wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika Shetani ni adui aliye dhahiri kwa mtu.

وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِنْ تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ آلِ يَعْقُوبَ كَمَا أَتَمَّهَا عَلَىٰ أَبَوَيْكَ مِنْ قَبْلُ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ {6}

Na kadhalika Mola wako atakuteua na atakufundisha tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema yake juu yako na juu ya ukoo wa Ya’qub; kama alivyowatimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako ni Mjuzi, Mwenye hekima.