read

Aya 16-20.: Wakaja Kwa Baba Yao Wakilia

Wakaja kwa baba yao usiku wakilia. Kwa kuvunga na kuyafinika waliyoyafanya. Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana mbio na tukamwacha Yusuf kwenye vitu vyetu, basi mbwa mwitu akamla.

Kuna mithali inayosema “Damu ya Yusuf iko mbali na mbwa mwitu.” Imeelezwa kuwa msimulizi mmoja alikuwa akiwasimulia watu kisa cha Yusuf. Alipofika mahali pa mbwa mwitu, akasema mbwa mwitu aliyemla Yusuf anaitwa fulani. Wakasema waliokuwepo: Yusuf hakuliwa na mbwa mwitu! Akasema msimulizi: Basi naliwe hili ni jina la mbwa ambaye hakumla Yusuf.

Na wewe hutatuamini, ijapokuwa tunasema kweli.

Imam Ali (a.s.) anasema: “Inatosha kua ni adhabu kwa muongo kuwa akisema ukweli haaminiwi
Na wakaja na kanzu yake ina damu ya uongo.

Maana yako wazi, lakini wafasiri walipokosa la kusema wakatofautiana kuhusu damu, kuwa je, ilkuwa ya paa au ya mwanakondoo. Wengine wamaesema kuwa Ya’qub alipoona kanzu ya mtoto wake ni nzima, alise- ma: Sijawahi kuona mbwa mwitu mpole kuliko huyu aliyemla mwanangu bila ya kuirarua kanzu yake.

Ama sisi tunatosheka na kuwa Ya’qub alisema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kutenda jambo, lakini subira ni njema. Na Mwenyezi Mungu ndiye wakuombwa msaada kwa haya mnayoyasema.

Haya ndiyo yaliyoelezwa na wahyi kuhusu jawabu ya Ya’qub kuwaambia wanawe; wala hakuna dalili ya jengine.
Aya inaonyesha kuwa Ya’qub alitambua uongo wao kutokana na husuda yao kubwa kwa Yusuf. Lakini alisubiri na kumwachia mambo yake Mwenyezi Mungu.

Ukaja msafara.

Katika Tawrat Kitabu cha mwanzo imesemwa kwamba msafara wenyewe ulikuwa wa kizazi cha Ismail; yaani waarabu, kwa sababu nasabu yao inaishia kwa Ismail bin Ibrahim (a.s.).

Wakamtuma mchota maji wao. Yaani awaletee maji. Akatumbukiza ndoo yake.

Mchota maji alipomuona Yusuf alisema: Ee habari njema! Huyu hapa mvulana!

Anajipa habari yeye mwenyewe au anawapa jamaa zake. Basi wakamtoa kisimani wakamficha ili awe bidhaa.

Walimficha na watu ili jamaa zake wasimjue, wakamfanya mtumwa aliye katika jumla ya bidhaa zao za biashara.

Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayoyafanya.

Yaani anajua siri yao ya kumfanya mtumwa na hali yeye ni mtu huru.

Na wakamuuza kwa thamani duni kwa pesa za kuhisabiwa.

Wafasiri wengi wamesema kuwa watu wa zama hizo wakipima pesa, kikiwa kitu thamani yake ni kubwa na wakihisabu ikiwa thamani ni ndogo. Na kwamba kusemwa pesa zenye kuhisabiwa ni ishara ya uchache wa thamani waliyouzia.

Na walikuwa hawana haja naye.

Ndio wakafanya haraka kumuuza kwa bei ya kutupa ili waondokane naye wasije wakatuhumiwa wizi.

وَقَالَ الَّذِي اشْتَرَاهُ مِنْ مِصْرَ لِامْرَأَتِهِ أَكْرِمِي مَثْوَاهُ عَسَىٰ أَنْ يَنْفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا ۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُ مِنْ تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ {21}

Na yule aliyemnunua kule Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee makazi ya heshima, huenda akatufaa au tukamfaya mtoto. Na kama hivyo tulimkalisha Yusuf katika nchi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na mwenyezi Mungu ndiye mshindi katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ {22}

Na alipofikilia kukomaa kwake, tulimpa hukumu na elimu. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.