Aya 74-76: Ibrahim Anajadili Kuhusu Watu Wa Nuh
Basi hofu ilipomwondokea Ibrahim na ikawa ile bishara imemfikia, alianza kujadiliana nasi juu ya watu wa Lut.
Baada ya kujua Ibrahim hali halisi ya wageni wake na madhumuni yao alitulia, na akajawa na furaha yeye na mkewe, Sarah, kwa habari ya kupata mtoto na mjukuu. Lakini hakufurahishwa na habari ya adhabu ya watu wa Lut. Akawa anajadiliana naao.
Kundi kubwa la wafasiri, akiwemo Arrazi na mwenye Tafsir Al-Manar, wamesema kuwa Ibrahim hakujadili kuhusu watu wa Lut; isipokuwa alijadili kuhusu Lut akihofia kupatwa na adhabu. Wafasiri hao wametoa dalili kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:
قَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطًا ۚ قَالُوا نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَنْ فِيهَا ۖ لَنُنَجِّيَنَّهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ {32}
Lakini ilivyo, Aya hii waliyoitolea ushahidi, haina uhusiano wowote na mjadala wa wa Ibrahim; isipokuwa ni kutolea habari tu kwamba humo yumo Lut; na ndio maana wakasema tunajua sana.
Ayah hii tunayoifasiri inazungumzia mjadala kuhusu watu wa Lut sio kwa Lut peke yake. Kuongezea kauli yake Mwenyezi Mungu:
Na hakika wao itawafikia adhabu isiyorudishwa.
Dhamir katika hakika wao na itawajia inawarudia watu wa Lut ambao ibrahim amewajadili. Lakini wafasiri wakasema kuwa kuwajadili watu wa Lut ni kumkosea Adabu Mwenyezi Mungu, na Ibrahim ni Maasum, kwa hiyo hapana budi iwe ni kujadili Lut pekee.
Nasi tunasema: Kwanza, hakuna tofauti katika kumjadili Lut peke yake au kaumu yake. Kujadili ni kujadili tu.
Pili, Mjadala ulikuwa unahusiana na kuondolewa adhabu waja wa Mungu au kuchelweshwa. Kwa hiyo hilo si dhambi; bali ni kinyume cha hivyo. Kwa sababu mjadala huu hauna kupingana wala kuzozana; isipokuwa ni kutaka hurumma kutoka kwa mwenye nguvu kwenda kwa mnyonge. Ombi hili linafahamisha upole na hurumma.
Ndio maana Mwenyezi Mungu akamsifu kuwa ni Mpole, mwenye hurumma mwepesi wa kurejea (kwa Mungu) baada ya kuwahurumia watu wa Lut
Tatu, Ibrahim alijadili kuhusu watu wa Lut ili awe na yakini kwamba wao wameasi kiasi ambacho hakuna tamaa ya kuongoka kwao; sawa na alivyosema:
قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِنْ ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَٰكِنْ لِيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ {260}
Hili linasisitizwa na kauli yake Mwenyezi Mungu:
Ewe Ibrahim! Achana nayo haya. Hakika amri ya Mola wako imekwishakuja, na hakika wao itawafikia adhabu isiyorudishwa.
Yaani usiniulize ewe ibrahim katika mambo yanayohusu watu wa Lut, kwa vile wao wataangamia tu, kwa sababu ya kuendelea kwao na shirk na ufisadi na kutokuwepo tama ya kutubia.
وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ {77}
وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِنْ قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَاتَّقُوا اللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنْكُمْ رَجُلٌ رَشِيدٌ {78}
قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِيدُ {79}
قَالَ لَوْ أَنَّ لِي بِكُمْ قُوَّةً أَوْ آوِي إِلَىٰ رُكْنٍ شَدِيدٍ {80}