read

Aya 84-86: Shuaib

Maana

Na kwa Wamadian (tulimpeleka) ndugu yao Shuaib. Akasema: Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, hamna Mungu mwingine zaidi yake.

Imepita tafsiri ya Aya hii kwa herufi zake katika Juz. 8 (7:85).

Wala msipunguze kipimo na mizani.

Hili ni katazo la kupunja; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

وَيْلٌ لِلْمُطَفِّفِينَ {1}

الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ {2}

“Ole wao wanopunja. Ambao wanapojipimia kwa watu hutaka watimiziwe. Na wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.” (83:1-2)

Mimi ninawaona mko katika kheri.

Makusudio ya kheri hapa ni riziki nyingi.

Na mimi nawahofia na adhabu ya siku izungukayo.

Hii ni kuwaonya na adhabu, kama wataendelea na maasi

Enyi watu wangu! Timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu.

Baada ya kuwakataza kupunguza sasa anawaamrisha kutimiza vipimo. Maana zote mbili ni sawa. Hatufahamu lengo lake zaidi ya kuwa ni kusisitiza tu.

Wala msiwatilie kasoro watu vitu vyao.

Vitu ni kila kitu; kama vile haki ya kimaada (yakuonekana) na ya kimaana (isyoonekana). Kwa hiyo ni haramu kumpunguzia mtu kitu au jambo lolote; kama ilimu yake na hulka yake.

Wala msifanye ufisadi katika nchi mkafanya vurugu.

Katika Aya hii kuna maneo mawili (tathaw na Mufsidin) yenye maana moja, ya ufisadi. Kwa hiyo ikawa ni lazima kufanya T’awil (tafsir inayowakilisha). Ama kutafsir Ta’athaw kwa maana ya juhudi; yaani msifanye juhudi ya kuleta ufisadi; au kutafsir Mufisidin kwa maana ya kuleta vurugu; kama vile vita na umwagaji damu, bila ya sababu inayowajibisha. Lakini vita vyenyewe vikiwa ni vya kuondoa ufisadi, basi itakuwa kuacha kupigana ndio ufisadi. Hapo Ndipo jihadi inakuwa ndio twaa bora. Taawili hii ni bora kuliko ile ya kwanza.

Alivyowabakishia Mwenyezi Mungu ni bora kwa ajili yenu ikiwa nyinyi ni waumini.

Halali ni njema na yenye kubaki hata ikiwa chache na haramu ni uovu, ni shari na inakwisha hata ikiwa nyingi. Tukichunguza sababu ya vita leo, tutaona ni kujilundikia mali wachache na kunyimwa wengi.

Imetokea sadfa kusoma magazeti ya leo 24-12-1968, kwamba jamaa huko London walifanya maandamano kuelekea makao ya mfalme, Birmingham (Birmingham Palace) wakimtaka malkia aiache ikulu yake, inayoweza kukaliwa na watu elfu, ambapo London pekee ina watu elfu sita wasio na makazi.
Wala mimi si mlinzi wenu wa kuwazuia na maasi kwa nguvu.

Umuhimu wangu ni kuwanasihi na kufikisha tu, na nimekwishatekeleza kwa ukamilifu na nimeondokana na majukumu. Shuaib (a.s.) ndiye anayesema hivyo.

قَالُوا يَا شُعَيْبُ أَصَلَاتُكَ تَأْمُرُكَ أَنْ نَتْرُكَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا أَوْ أَنْ نَفْعَلَ فِي أَمْوَالِنَا مَا نَشَاءُ ۖ إِنَّكَ لَأَنْتَ الْحَلِيمُ الرَّشِيدُ {87}

Wakasema: Ewe Shuaib! Je, Swala yako inakuamuru tuyaache waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu au kufanya tupendavyo katika mali zetu? Hakika wewe ndiwe mpole, mwongofu!

قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِنْ كُنْتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّي وَرَزَقَنِي مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّهِ ۚ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ {88}

Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa nina dalili iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu na ameniruzuku riziki njema itokayo kwake? Wala sipendi kuwakhalifu nikafanya yale ninayowakataza. Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyoweza. Na taufiki yangu haiko ila kwa Mwenyezi Mungu. Kwake ninategemea na kwake naelekea.

وَيَا قَوْمِ لَا يَجْرِمَنَّكُمْ شِقَاقِي أَنْ يُصِيبَكُمْ مِثْلُ مَا أَصَابَ قَوْمَ نُوحٍ أَوْ قَوْمَ هُودٍ أَوْ قَوْمَ صَالِحٍ ۚ وَمَا قَوْمُ لُوطٍ مِنْكُمْ بِبَعِيدٍ {89}

Na enyi watu wangu! Kupingana nami kusije kukawapelekea yakawasibu kama yaliyowasibu kaumu ya Nuh au kaumu ya Hud au kaumu ya Swaleh, na kaumu ya Lut si mbali nanyi.

وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ {90}

Na muombeni maghufira Mola wenu kisha mtubie kwake. Hakika Mola wangu ni Mwenye kurehemu, Mwenye upendo.