read

Aya 91-95: Lau Si Jamaa Yako Tungekurujumu

Maana

Wakasema: Ewe Shuaib! Hatufahamu mengi ya hayo unayoyasema.

Walifahamu vizuri amri, makatazo makemeo na ahadi alizowaambia, isipokuwa walikusudia, kwa kauli yao hii, kwamba vitisho na ahadi walizopewa na Shuaib si lolote kwao.

Kwa vile eti wao ni wasafi. Ibada yao ya masanamu ni safi kwa sababu waaliifanya mababu zao; na kupunja katika vipimo ni kusafi kwa vile ni demokrasia. Kwa hiyo madai ya Shuaib kwao ni kuvuruga amani ya uhuru wao.

Hayo ndiyo maneno ya wanyang’anyi kila mahali na kila wakati. Wanaua na kunyang’anya mali za watu; ukiwaambia wanasema tunataka kuleta amani na demokrasia na wewe unataka kuleta vurugu, kusababisha vita na kuvuruga amani. Kwa sababu amani, wanavyotaka wao, ni kuupigia magoti uovu wao na kusujudia masanamu yao.

Na sisi tunakuona kwetu ni mdhaifu Hakuna wakutuzuia kukukamata, kwa hiyo bora unyamaze.

Na lau si jamaa zako, bila shaka tungelikurujumu.

Unaweza kuuliza: imekuwaje kusema kuwa Shuaib ni mdhaifu, lakini watu wake wana nguvu; kwani nguvu za watu wa mtu si ndio nguvu zake?

Jibu: Hakuna kufanana kati ya nguvu mbili; huenda nguvu za watu wa mtu ni dhidi yake sio za kumsaidia yeye. Makuriash walikuwa ndio maadui wakubwa zaidi wa Muhammad mkuraishi.

Baadhi ya wafasiri wanasema kuwa kauli ya lau si jamaa zako, ina maana ya lau si kuwaheshimu jamaa zako. Tamko la Aya linakubaliana na maana haya.

Akasema: Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu?

Ni ajabu gani ya ujinga huu na upotevu?

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ {28}

“Hakika wanomwogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale tu wenye elimu” (35: 28).

Na Yeye mmemuweka nyuma ya migongo yenu?

Yaani mmemsahau na kumpuuza.

Enyi watu wangu! Fanyeni muwezavyo, mimi ninafanya niwezavyo.

Huu ni mfano wa kauli yake:

لِي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ ۖ أَنْتُمْ بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِمَّا تَعْمَلُونَ {41}

“Mimi nina amali yangu na nyinyi mna amali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa ninayoyatenda na mimi sina jukumu kwa mnayoyatenda.” Juz. 11 (10:41).

Na pia kauli yake:

لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ {6}

“Mna dini yenu nami ninadini yangu” (109:6).

Karibuni mtajua ni nanai itakayemfika adhabu itakayomfedhehesha na nani aliye mwongo. Na ngojeni nami ninangoja pamoja na nyinyi.

Hili ni karipio kutoka kwa Shuaib kwa watu wake kuwa watashukiwa na adhabu. Na hakuna dalili kubwa zaidi, inayofahamisha utume wake, kuliko kuamini ghaibu hii.

Ilipofika amri yetu tulimwokoa Shuaib na walioamini pamoja naye, kwa rehema itokayo kwetu. Na ukelele ukawaangamiza wale waliodhulumu, wakapambaukiwa wameanguka kifudifudi katika majumba yao. Kama kwamba hawakuwemo humo. Ehee! (watu wa) Madyan wamepotelea mbali; kama walivyopotelea mbali (watu wa) Thamud.
Umekwishapita mfano wa Aya hii katika Aya 66-67 ya Sura hii.

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُبِينٍ {96}

Na hakika tulimtumma Musa pamoja na Ishara zetu na dalili zilizo wazi

إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ {97}

Kwa Firauni na waheshimiwa wake, lakini wao walifuata amri ya Firauni na amri ya Firauni haikuwa yenye uongofu.

يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ ۖ وَبِئْسَ الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ {98}

Siku ya Kiyama atawatangulia watu wake na atawaingiza motoni. Ni pabaya mno mahala pa kufikiwa.

وَأُتْبِعُوا فِي هَٰذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ بِئْسَ الرِّفْدُ الْمَرْفُودُ {99}

Na wamefuatishiwa laana katika (dunia) hii na siku ya Kiyama ni kibaya mno watakachopewa.