read

Aya Ya 24-29: Alimtamani Naye Akamtamani

Lugha

Amesema Tabrasi, katika Majmaul-bayan kuwa neno hamma (lililofasiriwa kwa maana ya kutamani) lina maana nyingi. Miongoni mwanzo ni kuazimia, kupitia na mawazo bila ya kuazimia, kutamani kitu nk.

Na hakika (mke) alimtamani naye alimtamani kama asingeona dalili ya Mola wake.

Tumezungumzia, katika Juz.1 (2:35-39) na 124. Vile vile Juz.5 (4:58-59), kuhusu isma (kuhifadhiwa na dhambi) ya mitume na kwamba mitume wote ni wenye kuhifadhiwa na dhambi. Hapo linakuja swali, kuwa Yusuf ni mwenye kuhifadhiwa na dhambi kwa sababu yeye ni mtume. Na kauli yake Mwenyezi Mungu:
Naye alimtamani, inaonyesha azma mbaya ya kuitikia matamanio ya mke wa waziri. Imekuwaje?

Wafasiri wamejibu kwa majibu ya kufedhehesha, wengine wakatoka nje ya dhahiri ya maneno. Jawabu lililo karibu zaidi na dhahiri ya maneno na heshima ya mitume ni lile lisemalo kuwa katika Aya kuna kutangulizwa maneno na kuja nyuma. Asili yake ni: Na hakika (mke) alimtamani naye kama asingeona dalili ya Mola wake angelimtamani. Yaani hakumtamani kabisa; kama vile kusema: alikuwa amekwisha yule kama si fulani.

Ubainifu wa pili ni: Mambo yote yalikuwa tayari. Mwanamke amejileta mwenyewe; kijana naye amekamilika kuwa mwanamume, wako peke yao, hakuna wa kuwasikia wala wa kuwaona. Lakini kulikuwa na kizuizi kimoja tu, kilichomzuia Yusuf, chenye nguvu kuliko makemeo yoyote na kikubwa zaidi ya kila anayesikia na anayeona.

Nacho ni kujua kwake halali ya Mwenyezi Mungu na haramu yake na yakini yake kwamba Mwenyezi Mungu yuko karibu naye zaidi kuliko kuliko mshipa wa shingo; na kwam- ba yeye Mungu anajua zaidi kilicho moyoni na kilichojificha.

Hiyo ndiyo dalili iliyomzuia Yusf na kufikiria haram na inayomzuia kila mwenye kumwamini kikwelikweli Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, awe mtume au sio mtume.

Kuna wengine wamesema kuwa Yusuf haikumdhihirikia dalili ya Mola wake ila alipomtamani. La hasha! Haiwi hivyo kwa mitume na wakweli. Hakika dalili ya Mwenyezi Mungu, haiondoki kwa wauminii wakweli.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa ili tumwepushie uovu na uchafu. Hakika yeye ni katika waja wetu waliotakaswa.

Uovu ni vitimbi vya mke wa waziri na uchafu ni zina. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaomcha ambao wanamkimbilia kwake wakiwa ni wenye ikhlasi; anawalinda na kuwahifadhi na kila anayewakusudia uovu au anyejaribu kuwaingiza kwenye upotevu; sawa na alivyofanya Yusuf, alikimbilia kwa Mola wake, huku akisema:

“ Na kama hutaniondolea vitimbi vyao nitawaelekea na nitakuwa miongoni mwa wajinga Basi Mola wake akamwitikia na akamuondoshea vitimbi vyao. Kama Hakika yeye ni msikizi Mjuzi”

Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke akairarua kanzu yake kwa nyuma.

Yusuf alijaribu kumponyoka kwa kutoka pale nyumbani. Mwanamke naye akamfuatia nyuma, kama ngamia mkali, akamuwahi kabla ya kufika mlangoni, akamvuta kanzu yake kwa nyuma hadi ikachanika. Mara mume naye akaingia.

Wakamkuta bwana wake mlangoni.

Mwenye Tafsir Al-Manar anasema: “Wanawake wa Misri walikuwa wakiwaita waume zao bwana (sayyid) na hilo linaendela hadi leo.

Mume alipoingia nyumbani alimkuta Yusuf mlangoni alipomuona Yusuf amesimama mlangoni, huku kanzu yake ikiwa imeraruka; kabla ya kuuliza habari yoyote Akasema:

Hapana malipo ya mwenye kukusudia uovu kwa mkeo isipokuwa kufungwa gerezani au kupewa adhabu iumizayo.

Mke aliyasema haya kwa utulivu bila ya kuonyesha fadhaiko lolote. Anasema hapana malipo ya mwenye kukusudia uovu, nayeye mwenyewe ndiye muovu anayeutuhumu wema na usafi. Hii inatukumbusha wale ambao leo wameanzisha vita huko Vietnam, Mashariki ya kati, Kongo na kwengineko.

Na wanawapa silaha mabeberu ili wawamalize wanyonge huko Angola, Afrika kusini, Rhodesia (sasa ni Zimbwabwe), Latin Amerika na kwengineko. Wanaweka vituo vya kijeshi ardhini kote, mashariki na magharibi vikiwa na kila aina ya silaha za maangamizi.

Wanayafanya yote hayo kwa madai ya kuhifadhi amani na kuchunga haki za binadamu. Kwa hiyo hakuna ajabu kwa mwanamke huyo kuficha uongo wake kwa mumewe ili afiche makosa yake.

Akasema (Yusuf): Yeye ndiye aliyenitaka bila ya mimi kumtaka.

Nimejizuia naye na nikamkimbia akanipata hapa mlangoni akaifanyia hivi nguo yangu.

Na shahidi, aliyekuwa katika jamaa za mke, akatoa ushahidi.

Wafasiri wamerefusha maneno kuhusu shahidi huyu. Wengine wamesema ni binamu yake, wengine wakasema ni katika jamaa za mume na wengine wakasema alikuwa mtoto mchanga. Ama sisi tunasimama kwenye dhahiri ya wahyi amabo unafahamisha kuwa shahidi alikuwa ni katika jamaa za mke na alikuwa ni baleghe, kutokana kauli yake:

Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele, basi mke ni mkweli na yeye Yusuf ni katika waon- go na ikiwa kanzu yake imechanwa nyuma basi mke ni muongo na yeye Yusuf ni katika wakweli.

Haya ndiyo yaliyosemwa na wahyi. Ama kuwa shahidi alikuwa nani, alitoa vipi huo ushahidi, alikuja tu yeye mwenyewe au aliitwa na mengineyo, haya yamenyamaziwa na wahyi. Kuna hadith isemayo: “Mwenyezi Mungu ameyanyamazia mambo, basi msijikalifishe nayo.”

Basi mume alipoona kanzu imechanywa nyuma, alisema: Hii ni katika vitimbi vyenu (wanawake). Hakika vitimbi vyenu ni vikuu.

Mume alikinai na akawa na yakini ya ukweli wa Yusuf (a.s.) na uongo wa mkewe, lakini akaona asitri aibu. Akatosheka na kusema: Hakika vitimbi vyenu ni vikuu.

Wasifu huu unawapendeza wanawake, kwa sababu unaonyesha werevu wao na kwamba wanaume hawawezi kwa kwa hila na vitimbi.

Unaweza kuuliza: Hapa imesemwa kuwa vitimbi vya wanawake ni vikuu na katika Juz.5 (4:76), imesemwa kuwa vitimbi vya shetani ni dhaifu; je maana yake ni kuwa mwanamke ana nguvu kuliko shetani?

Jibu: Vitimbi vya wanawake ni sehemu ya vitimbi vya shetani. Mkusudio ya kuwa vitimbi vya shetani ni dhaifu ni kuwa shetani hana nguvu kwa waja wa Mwenyezi Mungu; isipokuwa yule mwenye kumfuata katika wapotevu. Na makusudio ya kuwa vitimbi vya wanawake ni vikuu ni kuwa wao ndio askari wa shetani wenye nguvu zaidi. Imepokewa kutokana na iblis kwamba yeye amesema: “Ninapochachiwa na laana za watu wema huwaendea wanawake kujiliwaza…”

Kisha waziri akasema: Yusuf! Achana nayo haya. Yaani yafiche haya wala usimwambie mtu. Na akamwambia mkewe: Na wewe mwanamke omba msamaha kwa dhambi zako, hakika wewe ni miongoni mwa wakosaji.

Hii ni dalili mkataa kwamba mume alikuwa na hakika kuwa Yusuf hakuwa na makosa, na mkewe ndiye mwenye makosa. Abu Hayan Al-andalusi (mhispania) katika tafsir yake Albahrul-muhit anasema: “Waziri hakuwa na wivu mwingi na hii ni tabia ya watu wa Misr” Naye mwenye tafsir Al- Manar akamjibu: “Haya ni maneno ya kujisemea yasiyokuwa ya kielimu sahihi.” Nasi tunaongeza kuwa hiyo imesababishwa na hawa na ubinafsi.

Neno wakosaji hapa kwa kiarabu limetumika kwa khatwiin dhamiri inay- otumika kwa wote wanaume na wanawake kwa sababu makosa yanatokea kwa wote.

Hukumu Kwa Ushahidi Wa Mazingira

Makusudio ya shahidi katika neno: ‘Na akashuhudia shahidi’ sio kuwa ni sharia kuchukua ushahidi wa aina hii; isipokuwa ni ujuzi wa kujua mambo yasiyojulikana. Kuchanika kanzu kunajulikana wazi na ni kawaida mtu akishikwa kwa nyuma, kanzu yake itachanika kwa nyuma, na akishikwa kwa mbele itachanika kwa mbele. Hapo anajulikana mkweli na muongo. Kwa mnasaba huu tunaashiria kuwa kuna aina tatu za kujua uhakika wa mambo:

1. Mambo yasiyokubalika kiakila; kwa mfano, mtu mwenye umri wa miaka arubaini kudai kuwa yeye ni mzazi wa mtu aliye na umri kama wake. Au kudai kuwa amerithi jengo fulani na inajulikana kwamba baba yake alikufa fukara. Madai kama haya na mfano wake, hayahitaji nukuu ya sharia katika kuyapinga.

2. Yanayotumika na kutegemewa na sharia; kama, kukiri makosa, ushahidi wa mwenyewe, ushahidi wa waadilifu wawili. Aina hii huitwa ‘ubainifu wa kisharia’ na katika sheria za kutungwa, wanaita: ‘ushahidi wa kikanuni.’ Wameafikiana wote kuwa ni wajibu kwa kadhi kuhukumu kulingana na nukuu za kisharia. Iwe ana uhakika au la.

3. Ushahidi wa kimazingira. Kutoa hukumu kwa ijtahadi yake na werevu wake kwa kulinganisha hali na mambo yanayoyazunguka madai. Kila madai yana mambo yake na hali zake na kila kadhi ana fahamu yake na ijtihadi yake. Miongoni mwa ulinganisho ni: ikiwa kanzu ime chanika kwa mble. Vile vile yale yaliyonasibishwa kwa Nabii Suleiman bin Daud (a.s.), au Imam Ali (a.s.) alipohukumu baina ya wanawake wawili waliokuwa wakigombania mtoto mmoja, kila mmoja akisema ni wake; akasema nipeni kisu nimpasue katikati, mmoja akakataa na mwengine akakubali, akampa mtoto yule aliyekataa.

La kushangaza katika niliyoyasoma kuhusiana na maudhui haya ni kauli ya Shatibi katika Kitabu almuwafiqat Juzuu ya pili uk. 267 suala la 11: “Abu bakar alitekeleza wasia wa ndoto” Yaani mtu alikufa na hakuwahi kuusia katika uhai wake, kisha akaufikisha wasia wake kwa anayemtaka kwenye usingizi na Abu bakar akaupitisha wasia huo.

وَقَالَ نِسْوَةٌ فِي الْمَدِينَةِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ تُرَاوِدُ فَتَاهَا عَنْ نَفْسِهِ ۖ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا ۖ إِنَّا لَنَرَاهَا فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ {30}

Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa mheshimiwa anamtaka mtumishi wake pasipo kutamaniwa naye. Hakika amegubikwa na mapenzi. Sisi hakika tunamuona yuko katika upotevu uliodhahiri.

فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ مُتَّكَأً وَآتَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ اخْرُجْ عَلَيْهِنَّ ۖ فَلَمَّا رَأَيْنَهُ أَكْبَرْنَهُ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَاشَ لِلَّهِ مَا هَٰذَا بَشَرًا إِنْ هَٰذَا إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ {31}

Aliposikia vitimbi vyao. Aliwaita na akawawekea matakia, na akampa kila mmoja wao kisu. Akasema: Tokea mbele yao. Walipomuona wakaona ni kitu kikubwa na wakakata mikono yao Na wakasema: “Hasha lillahi! Huyu si mtu, hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu.

قَالَتْ فَذَٰلِكُنَّ الَّذِي لُمْتُنَّنِي فِيهِ ۖ وَلَقَدْ رَاوَدْتُهُ عَنْ نَفْسِهِ فَاسْتَعْصَمَ ۖ وَلَئِنْ لَمْ يَفْعَلْ مَا آمُرُهُ لَيُسْجَنَنَّ وَلَيَكُونًا مِنَ الصَّاغِرِينَ {32}

Akasema (yule bibi): Huyu ndiye mliyekua mkinilaumia. Hakika nilimtaka kinyume cha nafsi yake, lakini akakataa. Na akitofanya ninayomwamrisha basi hapana shaka atafungwa gerezani na atakuwa miongoni mwa madhalili.

قَالَ رَبِّ السِّجْنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدْعُونَنِي إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا تَصْرِفْ عَنِّي كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُنْ مِنَ الْجَاهِلِينَ {33}

Akasema: Ewe Mola wangu! Gereza linapendeza zaidi kwangu kuliko haya wanayoniitia. Na kama hutanion- dolea vitimbi vyao nitawaelekea na nitakuwa miongoni mwa wajinga.

فَاسْتَجَابَ لَهُ رَبُّهُ فَصَرَفَ عَنْهُ كَيْدَهُنَّ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ {34}

Basi Mola wake akamwitikia na akamuondoshea vitimbi vyao; hakika yeye ni Msikizi, Mjuzi.

ثُمَّ بَدَا لَهُمْ مِنْ بَعْدِ مَا رَأَوُا الْآيَاتِ لَيَسْجُنُنَّهُ حَتَّىٰ حِينٍ {35}

Kisha ikawadhihirikia baada ya kuona ishara ya kuwa wamfunge kwa muda.