read

Surah Ya Kumi na Mbili: YUSUF

Sura hii imeshuka Makka. Tabrasi akimnukuu Ibn Abbas, anasema kuwa kuna aya nne zilizoshuka Madina ambazo ni: 1,2,3,8.Ina Aya 111.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ {1}

Alif laam raa. Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha

إِنَّا أَنْزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ {2}

Hakika sisi Tumeiteremsha Qur’ani kwa kiarabu ili mpate kutia akilini.

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَٰذَا الْقُرْآنَ وَإِنْ كُنْتَ مِنْ قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ {3}

Sisi tunakusimulia simulizi nzuri sana kwa kukupa wahyi Qur’ani hii. Na hakika kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa wasio na habari.