read

Aya 1 – 2: Hizo Ni Aya Za Kitab Chenye Hekima

Maana

Alif Lam Ra.

Yametangulia maelezo kuhusu herufi hisi katika mwanzo wa Sura Baqara Juz.1

Hizo ni Aya za Kitab chenye hekima.

Hizo ni ishara kwamba kila Aya katika Aya za Qur’ani inakusanya hekima.
Je, imekuwa ni ajabu kwa watu, kwamba tumempa wahyi mmoja wao

Wapinzani waliona ajabu Mwenyezi Mungu kuwasiliana na mja miongoni mwa waja wake. Mshangao huu ulikuwa na sababu zifuatazo:-

1. Walimpima Muhammad (s.a.w.) na wao wenyewe, kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu hawasiliani na wao, basi inatakikana asiwasiliane na mwingine.

Jibu la hilo tunalipata katika Aya isemayo:

اللَّهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗ {124}


“Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi, zaidi wa kujua mahali anapoweka ujumbewake”Juz.8(6:124)

Yaani Muhammad (s.a.w.) ana sifa za kumwezesha kuchukua utume kuliko wengine.

2. Wao hawakujua aina ya mawasiliano na Mwenyezi Mungu, wakadhani kwamba kuwasiliana kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na Muhammad ni sawa na wanavyowasiliana wao kwa wao. Jibu la mawazo haya tunalipata katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَنْ يُكَلِّمَهُ اللَّهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِنْ وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا{51}


“NahaiwikwamtukusemanaMwenyeziMunguilakwawahyiaunyuma yapaziaauhumtumamjumbe…”(42:51)

Tatu: Kwamba Muhammad aliwaletea lile wasiloliitakidi wala kuzoweya. Na hili ndilo muhimu zaidi. Jibu lake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

قَالَ لَقَدْ كُنْتُمْ أَنْتُمْ وَآبَاؤُكُمْ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ {54}


“Akasema:Hakikanyinyinababazenumlikuwakatikaupotevuuliowazi” (21:54)

Kuwa uwaonye watu na uwape bishara wale walioamini kwamba wana cheo kikubwa mbele ya Mola wao.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kubainisha kustajabu kwa makafiri wahyi kwa Muhammad (s.a.w.), anabainisha hakika ya aliyoyatumia wahyi kuwa ni maonyo na bishara – kumuonya na adhabu kali yule anayehalifu na kuasi amri ya Mwenyezi Mungu na kumpa bishara ya thawabu yule anayefuata amri. Thawabu zimetajwa kwa ibara ya cheo kikubwa.

Ikiwa wahyi wenyewe ndio huu na Muhammad (s.a.w.) akawa na sifa za kuuchukua na kuufikisha, sasa yako wapi maajabu?

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hawezi kuwaacha watu bila ya kuwatumia mjumbe mwaminifu awafikishie wanayoyataka katika heri na wanayoyachukia katika shari, wajiepushe na hili na wafanye lile. Na pia ili wasiwe na hoja, kama wakihalifu. Na Muhammad (s.a.w.) ndiye mwaminifu wa ujumbe huu kuliko watu wengine. Kwa hiyo imepasa yeye awe ndiye mjumbe wa Mwenyezi Mungu.

Wakasema Makafiri: Hakika huyu ni mchawi aliye wazi.

Walimsifu Muhammad (s.a.w.) kwa uchawi, kwa vile wao waliikana Qur’ani kuwa ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Vile vile walishindwa kuleta Sura iliyo mfano wake. Kwa hiyo hawakubakiwa na jingine ila kudai uchawi tu. Walishindwa na wakajitia kushindwa kujua kuwa kila lililo katika Qur’ani ni hakika isiyo na shaka, na kwamba uchawi ni uwongo usio na msingi.

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِنْ شَفِيعٍ إِلَّا مِنْ بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ {3}


Hakik


a


Mol


a


wen


u


ni Mwenyez


i


Mung


u


ambaye ameumb


a


mbing


u


n


a


ardhi


katikasikusita,kishaakastawi


ju


uy


a


Arshi


.


Y


ey


ehutengenez


a


mambo


.


Hakuwa


mwombezi ila baada ya idhini yake. HuyondiyeMwenyezi


Mungu


,


Mol


a


wenu


,


basi


mwabuduni. Jehamkubuki?

إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ اللَّهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ بِالْقِسْطِ ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ {4}


Kwake ndiye marejeoyenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika yeye ndiye anayeanzisha kiumbe kisha


huki


r


ejesh


a


il


i


awalip


e


wale


walioamini na wakafanya amali njema kwa uadilifu. Na


waliokufuru


,


watapat


a


kiny


waji cha maji yachemkayo na adhabu chungu kwa kuwa walikuwawakikufuru.