read

Aya 100 – 102: Waliotangulia Wa Kwanza

Maana

Katika Aya hizi tatu Mwenyezi ametaja aina nne katika uma, kisha akaongezea aina ya tano katika Aya 106, tutaizungumzia tutakapofika huko. Ama aina nne ni hizi:

Na waliotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansari.

Wote (Wahajiri na Ansari) wamefanywa ni aina mbili zilizotangulia. Hakuna mwenye shaka kuwa makasudio ya kutangulia ni katika Hijra na Nusra (kuhama na kuwasaidia waliohama).

Sifa inatambulisha hivyo, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuelezea wakati wa huko kutangulia. Ndio maana wakatofautiana wafasiri: Kuna wenye kusema kuwa makusudio ni kuhama na usaidizi kabla ya siku ya Badr. Wengine wanasema kuwa ni kabla ya Baia ya Ridhwani iliyokuwa chini ya mti siku ya Hudaibia. Mwingine anasema ni wale walioswali Qibla mbili.

Tuonavyo sisi ni kwamba waliotangulia kuhama na kusadia (Muhajirin na Ansari) ni kabla ya waislamu kuwa na nguvu ya kuwazuia wanaowa- chokoza na kufitini dini yao; kama walivyofanya washirikiana mwanzo wa dawa.

Kwa hiyo basi kauli ya kwanza ndiyo yenye nguvu, kwa sababu nguvu ya waislamu ilidhihiri siku ya Badr walipohisi washirikina ukakamavu na nguvu ya Uislamu.

Na wale waliowafuata kwa wema.

Nao ni kila mwenye kwenda njia ya waliotangulia wenye ikhlasi. Anasema Tabrasi: Anaingia katika hao kila atakayekuja baada yao hadi Kiyama”.

Yamekuja maelezo ya waliowafuata kwa wema katika Aya isemayo:

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِنْ بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ {10}


“Na wale waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu!T


ughufurie sisi na ndugu zetu waliotutangulia katika imani wala usijaalie katika nyoyo zetu mfundo kwa walioamini. Mola wetu! Hakika wewe ni Mpole sana Mwenyekurehemu”(59:10).

Tunataraji watapata funzo kwa Aya hii wale wanaotoa mwito wa imani na huku wenyewe wamejawa na mifundo ya hasadi.

Aina mbili hizi – waliotangulia na waliowafuatia – ndio ambao Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi naye na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele.

Mwenyezi Mungu yuko radhi nao kwa twaa yao na ikhlasi yao, na wao wako radhi naye kwa neema alizowamiminia.

Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Yaani hakuna kufuzu kwa maana yake sahihi ila kwa radhi ya Mwenyezi Mungu.

Utauliza! Dhahiri ya Aya inaonyesha kule tu kutangulila kwa kuhama na kusaidia, kunatosheleza kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kwamba huo ni wema usiodhuriwa na uovu. Sasa je, dhahiri hii, ni hoja kiasi ambacho ni wajibu kwetu kumtukuza kila aliyetangulia kwa Hijra na Nusra, hata kama yamethibiti kwake maasi?

Jibu: Makusudio ya waliotangulia wa kwanza ni wale waliomtii Mwenyezi Mungu na wakafa juu ya sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.).

Ama wale waliomwasi na wakafanya uovu baada ya kutangulia hawachanganywi na walio na radhi ya Mwenyezi Mungu; vipi iwe hivyo na hali yeye Mwenyezi Mungu anasema:

مَنْ يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا {123}


“Mwenye kutenda uovu atalipwa kwa ovu huo.


W


ala hatajipatia mlinzi walamsaidizizaidiyaMwenyeziMungu.”Juz.5(4:123)

لِيَجْزِيَ اللَّهُ كُلَّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ {51}“IliMwenyeziMunguailipekilanafsikwayaleiliyoyachuma. Hakika MwenyeziMungunimwepesiwakuhisabu”(14:51).

Na amepokea Bukhari, katika sahih yake Juz.9 Kitabu Alfitan mlango wa kwanza, Hadith isemayo:

“Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) atasema siku ya Kiyama: Hao ni swahaba zangu. Naye ataambiwa: Hujui walifanya nini baada yako. Hapo nitasema: Ole wake! Ole wake, mwenye kuibadilisha (dini yake) baada yangu”1

Hakuna mwenye shaka kwamba waliotangulia katika kuhama na kusaidia wahamiaji wana ubora, lakini hili ni jambo jingine na kusamehewa maasi au kuwa wasihisabiwe ni jambo jingine.

3. Na miongoni mwa mabedui walio pambizoni mwenu wamo wanafiki na katika wenyeji wa Madina wako waliobobea katika unafiki. Huwajui, sisi tunawajua.
Amekwisha taja Mwenyezi Mungu (s.w.t.) wanafiki katika Aya kadhaa. Hapa anawataja kwa mnasaba wa kuwataja waumini waliotangulia; na ili kumpa habari Mtume wake mtukufu sehemu walikokwamba wao wamemzunguka kila upande.

Wako Madina anapokaa yeye na vitongojini mwake, sehemu za jangwani. Na kwamba wanafiki wa Madina ni mahodari katika fani ya unafiki kiasi cha kuweza kuuficha kwa Mtume pamoja na kuwa nao wakati mwingi. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anabainisha malipo ya wanafiki kwa kauli yake:

Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.

Adhabu hii ya mwisho ambayo watarudishwa ni maarufu, Jahanamu. Ama aina na wakati wa adhabu ya mara ya kwanza na ya pili kabla ya adhabu ya Jahanamu, haikuashariwa na Aya.

Sio mbali kuwa adhabu ya mara ya kwanza ni wakati wa kufa kwa sababu ya kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ يَتَوَفَّى الَّذِينَ كَفَرُوا ۙ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ {50}


“Na lau ungeliwaona Malaika wanapowafisha wale waliokufuru wakipiga nyuso zao na migongo yao na (kuwaambia) ionjeni adhabu iunguzayo” Juz.10(8:50)

Ama adhabu ya mara ya pili ni adhabu ya kaburi kutokana na Hadith nyingi kuwa kaburi ya kafiri ni shimo miongoni mwa mashimo ya Jahanamu, na kaburi ya mumin ni bustani katika bustani za peponi.

4. Na wengine wamekiri dhambi zao; wakachanganya vitendo vyema na vingine viovu.

Hawa ni wale waumini ambao mara kwa mara wanafanya mema kwa msukumo wa imani yao na mara nyingine hawaa hushinda imani yao wakafanya uovu, nao ni wengi. “Ni nani ambaye hulka zake zote zinaridhisha” isipokuwa wale waliohifadhiwa na Mola wako. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akabainisha hukumu ya hawa kwa kauli yake:

Huenda Mwenyezi Mungu akapokea toba zao kwa vile wao wametambua makosa na kuyakiri kwa hiyo wamekuwa, kwa hilo, ni mahali pa kutarajia rehema ya Mwenyezi Mungu na maghufira yake.

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Katika Majmaul-Bayan imeelezwa: “Wafasiri wanasema: ‘Huenda’ ikitoka kwa Mwenyezi Mungu inakuwa ni hakika; isipokuwa amesema ‘huenda’, ili wawe baina ya tamaa na wasibwete wakupuuza toba.

خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِمْ بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَهُمْ ۗ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ {103}


Chukuasadakakatikamali


za


o


uwasafish


e


na uwatakas


e


kwayo


.


Na


uwaombee


r


ehema. Hakika


maomb


i


yak


o


n


i


utulivu


kwao.NaMwenyeziMungu


niMsikizi,Mjuzi.

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ {104}


Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ndiye


anayekubal


i


tob


a


y


a


waja


wake na kuzipokea sadaka. Na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye ku


r


ehemu?

وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ ۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {105}


Na sema:


T


endeni vitendo Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini wataviona vitendo vyenu na mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghaibu na


dhahiri


,


nay


e


awaambie


mliyokuwamkiyatenda.

وَآخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ اللَّهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ {106}


N


a


wengin


e


wanangojea


amri ya Mwenyezi Mungu,


am


a


atawaadhib


u


au awakubali


e


toba


.


Na


Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenyehekima

  • 1. Hadith hii katika sahih Bukhari cha kingereza, ni Hadith no.174 uk.144. Pia ina- patikana katika sahihi Muslim Juz. 4 Uk. 1236, hadith no. 5682. -Mtarjumu